Sunday, July 10, 2016

MAANDAMANO YA WAMAREKANI WEUSI YAPAMBA MOTO.











Maandamano ya Wamarekani Weusi nchini Marekani kupinga mauaji ya wenzao wawili yamechukua sura mpya baada ya kuingia siku ya tano huku polisi wakiwa katika tahadhari kubwa kutokana na kuwepo tetesi za mipango ya mauaji ya polisi wengine.

Tahadhari hiyo imekuja ikiwa ni siku chache baada ya mauaji ya polisi watano katika Mji wa Dallas.

Waandamanaji wenye hasira wameendelea kuandamana huko Baton Rouge, Louisiana, ambapo mfanyabiashara wa mtaani Alton Sterling alikamatwa na kupigwa risasi na polisi wawili Jumanne asubuhi.

Katika maeneo kadhaa nchini humo polisi wameendelea kuwakamata wananchi hao.

Waandamanaji katika eneo la St Paul, Minnesota ambapo Mmarekani mwingine mweusi, Philando Castile aliuawa na polisi mzungu waliwatupia fashifashi na mawe polisi na kuwajeruhi watatu.

Sehemu nyingine ambapo maandamano yanaendelea ni New York, San Francisco, Denver, Florida, Pittsburgh, Philadelphia, Salt Lake City na Rhode Island.

0 Responses to “MAANDAMANO YA WAMAREKANI WEUSI YAPAMBA MOTO.”

Post a Comment

More to Read