Sunday, July 10, 2016
WANAWAKE WALIA MAGUFULI KUWABANIA KATIKA UTEUZI.
Do you like this story?
Mashirika
yanayotetea haki za wanawake na usawa wa kijinsi nchini yamesema uteuzi wa
nafasi muhimu za uongozi serikalini unaofanywa na Rais John Magufuli,
hauzingatii hali halisi ya uwakilishi wa kijinsia.
Akizungumza
jana jijini Dar es Salaam kwa niaba ya mashirika hayo, Mkurugenzi wa Mtandao wa
Jinsia Tanzania (TGNP), Lilian Liundi alisema licha ya kupiga kelele tangu
uteuzi wa Baraza la Mawaziri kuwa haukuzingatia usawa huo, bado hali inaonekana
kuwa tete kwa upande wa wanawake.
Alisema
katika baraza hilo, kati ya mawaziri 19, wanne pekee ndiyo wanawake sawa na
asilimia 21.1 ya mawaziri wote ikilinganishwa na uteuzi wa baraza la Serikali
ya Awamu ya Nne ambalo lilikuwa na mawaziri wanawake 10 sawa na asilimia 33.3.
Alisema
manaibu waziri kati ya 16 waliopo, wanawake ni watano sawa na asilimia 31.25.
“Ukiangalia
upande wa makatibu wakuu, walioteuliwa ni 29 kati ya hao, wanaume ni 26 sawa na
asilimia 89.7 huku wanawake wakipungua kutoka watano sawa na asilimia 21.7 ya
mwaka 2014 hadi kufikia watatu sawa na asilimia 10.3 kwa sasa,” alisema Liundi.
Alisema
uteuzi wa wanawake katika nafasi hizo umepungua kwa asilimia 10. Katika nafasi
ya wakuu wa mikoa, Liundi alisema idadi ya wanawake imeshuka zaidi, kati ya
wakuu wa mikoa 26 Tanzania Bara, 21 ni wanaume sawa na asilimia 80 na wanawake
ni watano sawa na asilimia mbili.
Kadhalika, alisema idadi ya wakuu wa wilaya imezidi kuporomoka ikilinganishwa na ya Februari mwaka jana ambako wanawake walikuwa asilimia 35.07: “Kwa maana nyingine, hapa uteuzi umepungua kwa asilimia saba.”
Liundi alisema mikoa mitatu ya Simiyu, Songwe na Singida haina wawakilishi wanawake kwa nafasi ya ukuu wa wilaya.
Kadhalika, alisema idadi ya wakuu wa wilaya imezidi kuporomoka ikilinganishwa na ya Februari mwaka jana ambako wanawake walikuwa asilimia 35.07: “Kwa maana nyingine, hapa uteuzi umepungua kwa asilimia saba.”
Liundi alisema mikoa mitatu ya Simiyu, Songwe na Singida haina wawakilishi wanawake kwa nafasi ya ukuu wa wilaya.
“Hii
iko hata kwenye nafasi za makatibu tawala wa mikoa na wilaya na wakurugenzi wa
halmashauri, hatuoni idadi ya wanawake ikiongezeka na badala yake inashuka,” alisema.
Mwakilishi
wa Taasisi ya Women Fund Tanzania (WFT), Dk Dinna Mbaga alisema Tanzania ni
kati ya mataifa duniani yaliyoridhia na kusaini mikataba mbalimbali ya kimataifa
na kikanda inayoweka misingi ya usawa kwa binadamu ikiwamo ushiriki katika
ngazi zote za uamuzi, lakini haitekelezi mikataba hiyo kwa ridhaa mpaka
isukumwe na asasi za kiraia jambo linaloleta ukakasi.
Alisema
miongoni mwa mikataba hiyo ni Tamko la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu
(UDHR: 1948), Mkataba wa Kimataifa wa Kutokomeza aina zote za Ubaguzi dhidi ya
Wanawake (CEDAW: 1979), Mpango kazi wa Beijing (1995), Mkataba wa Ziada wa
Maputo na Mkataba wa Nyongeza wa Jinsia na Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Mwakilishi
wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (Tamwa), Gladness Munuo
alisema Tanzania kupitia Dira ya Maendeleo ya 2025, imetambua kuwa mojawapo ya
vichocheo vya ukuaji wa uchumi ni pamoja na kuwa na jamii yenye maono ya kimaendeleo
na utamaduni wezeshi kwa wanawake na makundi mengine.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WANAWAKE WALIA MAGUFULI KUWABANIA KATIKA UTEUZI.”
Post a Comment