Thursday, July 31, 2014
BASI LAUA 17 KUMI NA KUMI NA MOJA WATAMBULIWA.
Do you like this story?
Watu
11 kati ya 17 waliofariki dunia papohapo katika ajali eneo la Pandambili
wilayani Kongwa, Dodoma wametambuliwa na wanne kati yao tayari wamechukuliwa na
ndugu zao.
Ajali
iliyosababisha watu 56 kujeruhiwa vibaya. iliyahusisha magari mawili ambayo ni
basi aina ya Scania mali ya Kampuni ya Morobest lililokuwa likitokea Mpwapwa
kwenda Dar es Salaam, ambalo liligongana na uso kwa uso na lori lenye tela,
lililokuwa limepakia shehena ya mabomba.
Ajali
hiyo ambayo ilisababisha vifo vya madereva wa magari hayo, ilitokea meta chache
kutoka mahali ilikotokea ajali iliyosababisha kifo cha aliyekuwa Mbunge wa
Tarime, marehemu Chacha Wangwe.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Dodoma David Misime aliielezea tukio hilo lilitokea saa 2
asubuhi kuwa miongoni mwa ajali mbaya ambazo zimetokea mkoani humo katika siku
za karibuni.
“Ni
watu 17 ambao wamekufa hapa hapa, kati ya hao 12 ni wanaume na wanawake ni
watano, majeruhi ni 56, kati yao tisa wana hali mbaya zaidi,” alisema Misime.
Hadi
jana jioni maiti za watu kumi na moja walikuwa wametambuliwa na wanne kati yao
walichukuliwa na ndugu zao.
Waliotambuliwa
ni Gabriel Lemanya (Dereva wa lori) ambaye ni Mkazi wa Ndebwe wilaya ya
Chamwino, Said Lusogo (dereva wa basi), Omari Mkubwa (kondakta wa basi) na
Mikdadi Zuberi ambaye alikuwa ni utingo wa lori.
Wengine
ni Justin Makasi, Gabriel Chiwipe, Marick Masawe na Melina Maliseli, Wilson
Sudai (wote wakazi wa Mpwapwa) watu wawili walitambulika kwa jina moja ambao ni
Christina (Mpwapwa) na Nasibu mkazi wa Kongwa.
Mashuhuda
walisema Polisi wa Kituo cha Kongwa walifika katika eneo la ajali muda mfupi tu
baada ya magari hayo kugongana na kwamba walisaidia kudhibiti usalama wa mali
za abiria, zikiwamo simu za mkononi zaidi ya 20 ambazo zilikabidhiwa kwa
uongozi wa polisi Mkoa wa Dodoma.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “BASI LAUA 17 KUMI NA KUMI NA MOJA WATAMBULIWA.”
Post a Comment