Thursday, July 31, 2014
MBEYA CEMENT YATOA MSAADA WA SARUJI 1000 UJENZI WA KIWANJA CHA MICHEZO CHUNYA.
Do you like this story?
Mkuu wa Wilaya Chunya Mkoani Mbeya Deodatus Kinawiro akitoa taarifa ya ujenzi wa kiwanda hicho |
Mtendaji mkuu wa kampuni ya saruji Mbeya (Lafarge)Catherin Langreney akitoa taarifa ya utoaji wa msaada huo |
(Picha na Fahari News)
Jumla ya
mifuko 1000 ya saruji sawa na tani 50 yenye thamani ya Sh15milioni imetolewa na
Kampuni ya saruji Mbeya (Mbeya cement)
kwa serikali Wilayani Chunya kwa ajili
ya ujenzi wa kiwanja cha kisasa cha
michezo Wilayani humo.
Ujenzi wa
kiwanja hicho Chunya unatarajia kugharimu kiasi cha fedha Sh 8bilioni ambapo
tayari ujenzi wake umeanza wilayani
ambapo Uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 50,000 pia unatarajiwa
kuwa kitega uchumi kwa halmashauri
ya wilaya ya Chunya na mkoa wa Mbeya.
Akizungumza
wakati wa kukabidhi saruji hiyo Mtendaji
Mkuu wa Mbeya Cement Catherine
Langreney alisema kuwa kampuni yake imepokea maombi hayo kutoka kwa Mkuu wa
wilaya ya Chunya na kukubali kuchangia saruji mifuko 1000 baada ya kugundua
kuwa uwanja huo utaweza kutoa ajira kwa vijana wengi na kuendeleza michezo.
Langreney
alisema kuwa ksmpuni hiyo imekuwa
ikichangia huduma mbalimbali za kijamii
kwa wananchi waliopo maeneo ya karibu na kiwanda hivyo, msaada huo ni sehemu ya
huduma zao za kawaida kwa wananchi.
Aidha
alisema kuwa uongozi wa kiwanda hicho unajipanga kutambulisha tekonolojia za
kujenga nyumba bora kwa gharama nafuu kwa lengo la kuwasaidia wananchi wenye
kipato cha chini.
Kwa upande
wake Mkuu wa Wilaya ya Chunya Deodatus Kinawiro alisema kuwa uwanja huo
unajengwa na wananchi wenyewe kwa kushirikiana na Halmashauri ya wilaya hiyo
ambapo pendekezo la ujenzi wa uwanja huo aliliwasilisha kwenye vikao vya
halmashauri na kuridhiwa na baraza la Madiwani.
Amesema
katika vikao vyake, ambapo Halmashauri ya wilaya hiyo ilipendekeza kutenga Sh
70milioni katika bajeti yake ya kila
mwaka huku kila mwananchi akiwajibika kuchangia ujenzi wa uwanja huo kuanzia
sh.2000 kwa kila mwaka ambapo matazamio uwanja huo unatarajia kukamilika 2016.
Amesema
kuwa fursa ya kuwepo kwa uwanja huo wa kisasa itainua michezo ndani ya wilaya
hiyo na mkoa wa Mbeya kwa ujumla hivyo wadau wanapaswa kujitokeza kuchangia
maendeleo ya uwanja huo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MBEYA CEMENT YATOA MSAADA WA SARUJI 1000 UJENZI WA KIWANJA CHA MICHEZO CHUNYA.”
Post a Comment