Friday, April 28, 2017
RC MAKALLA AUAGIZA UONGOZI WA WILAYA, JIJI, POLISI,SUMATRA, BODABODA, BAJAJI NA DALADALA KUKUTANA
Do you like this story?
Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akizungumza katika mkutano wake wa
kupokea kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi kwa utaratibu maalum
aliyojiwekea kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya
ya Mbeya William Ntinika.
wananchi wakiuliza maswali
Wakazi wa jiji la mbeya waliohudhuria mkutano huo.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akifafanua jambo kwa wanahabari.
MKUU
wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla amemeuagiza uongozi wa Wilaya, Jiji la
Mbeya,Polisi, Sumatrapamoja na viongozi wa Bajaji, Daladala na Bodaboda
kukutana na kuboresha namna ya utoajibhuduma ambao utaepusha ajali,
msongamano katika jiji hilo.
Makalla
amesema lazima jiji la Mbeya liwe safi na liwe la mfano katika kila
nyanya ikiwepo ya utoaji huduma ya usafiri kulinganisha na maemeo
mengine nchini.
Ameomba ushirikiano kwa viongozi, watendaji na wananchi kuunga Mkono jitihada hizo.
Katika
kuhakikisha hilo linafanyiwa kazi haraka, Makalla ameahidi kuitisha
mkutano muda wowote na wenyeviti na makatibu wa Mabaraza ya Ardhi ngazi
ya Wilaya kufuatia malalamiko mengi kuelekezwa kwenye Mabaraza ya
ardhi.
Mkuu
wa mkoa wa Mbeya ameyasema hayo leo wakati wa mkutano wa kusikiliza
kero za wananchi utaratibu ambao ameuweka tangu alipoteuliwa mwezi machi
mwaka jana ambapo Mkuu wa Mkoa husikiliza kero za wananchi mara mbili
kwa mwezi.
Utaratibu huu umepongezwa na wananchi na umesaidia sana kutatua kero nyingi za wananchi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “RC MAKALLA AUAGIZA UONGOZI WA WILAYA, JIJI, POLISI,SUMATRA, BODABODA, BAJAJI NA DALADALA KUKUTANA”
Post a Comment