Friday, April 28, 2017
KUTANA NA KISIWA CHA FAROE HAKINA WANAWAKE...WANAUME WAMEAMUA KUTAFUTA KWENYE MATAIFA MENGINE
Do you like this story?
Athaya Slaetalid na mumewe Jan pamoja na mwana wao Jacob
Kuna upungufu wa wanawake katika kisiwa cha Faroe.
Hivyo basi wanaume katika kisiwa hicho wanatafuta wanawake kutoka maeneo mengine kama vile mataifa ya Thailand na Ufilipino.
Lakini je ni changamoto gani zinazowakumba wanawake wanaoelekea katika kisiwa hicho.
Wakati Athaya Slaetalid alipoelekea katika kisiwa hicho ambapo kipindi
cha majira ya baradi huchukua muda wa miezi sita alikuwa akikaa karibu
na kikanza ama heater kwa jina la Kiingereza kwa siku nzima.
''Watu walikuwa wakiniambia niende nje kwa sababu kuna jua lakini nilisema'': ''Hapana niwacheni, nahisi baridi sana''.
Kuhamia katika kisiwa hicho miezi sita iliopita ilikuwa vigumu kwa Bi Athaya aliyekiri.
Alikutana na mumewe Jan alipokuwa akifanya kazi na rafikiye mmoja wa
kisiwa hicho ambaye alikuwa ameanza biashara nchini Thailand.
Jan alijua mapema kwamba kumpeleka mkewe katika utamaduni huo, hali ya hewa itakuwa changamoto kubwa
.
Kisiwa cha Faroe chenye upungufu wa wanawake
"Nilikuwa na wasiwasi kwa sababu kila kitu alichokiwacha nchini Thailand
kilikuwa tofauti na kile alichokuja kuona katika kisiwa cha Faroe'',
alisema.
''Lakini kwa sababu namjua Athaya nilijua ataingiliana na hali ya hewa''.
Kufikia sasa kuna takriban wanawake 300 kutoka Thailand na Ufilipino wanaoishi katika kisiwa cha Faroe.
Haionekani kuwa idadi kubwa lakini kisiwa hicho chenye idadi ya watu
50,000 sasa wanawakilisha watu walio wachache katika visiwa hivyo 18
kati ya Norway na Iceland.
Katika miaka ya hivi karibuni visiwa vya Faroe vimepata upungugufu wa wa
idadi ya watu huku vijana wakiondoka ili kutafuta elimu na huwa
hawarudi.
Wanawake wameamua kuishi ughaibuni.
Kulingana na waziri mkuu Axel Johannese, kisiwa hicho kina upungufu wa
jinsia huku kukiwa na uchache wa takriban wanawake 2000 ikilinganishwa
na wanaume.
Hatua hiyo imewafanya wanaume katika kisiwa hicho kutafuta wanawake katika maeneo mengine kwa mapenzi.
Wengi ijapokuwa sio wote wa wanawake hao wa bara Asia, walikutana na
wanaume zao kupitia mtandaoni wengine kupitia mitandao ya kukutanisha
wapendanao.
Wengine wamepatana kupitia mitandao ya wanandoa wa Asia na visiwa vya Faroe.
Kwa wale wanaowasili, utamaduni wa eneo hilo unaweza kuwaathiri.
Vikiwa ni miliki za Denmark, visiwa vya Faroe vina lugha yao na utamaduni wa kipekee hususan katika maswala ya chaku
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “KUTANA NA KISIWA CHA FAROE HAKINA WANAWAKE...WANAUME WAMEAMUA KUTAFUTA KWENYE MATAIFA MENGINE”
Post a Comment