Thursday, April 27, 2017
Nay wa Mitego apigwa onyo kali na Ustawi wa Jamii
Do you like this story?
Kutokana
na wanawake kadha wa kadha kujitokeza na kudai kwamba wamezaa na staa
wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ lakini amewatelekeza,
Idara ya Ustawi wa Jamii jijini Dar es Salaam, imemuonya jamaa huyo na
kumtaka kuwa makini katika hilo.
Ustawi
wa jamii wamesema suala la Nay kutelekeza watoto linaweza kumletea
matatizo kama vile kifungo jela au kulazimishwa kumlea mtoto husika hadi
akue na kuweza kujitegemea.
“Anachokifanya Nay siyo kitu kizuri kabisa kwani kwanza anawadhalilisha wanawake kwa kuzaa nao, halafu hawahudumii.
“Suala
la kutelekeza watoto linaweza kumsababishia kifungo au kutoa matumizi
kwa lazima kama wahusika, yaani wanawake waliozaa naye watachukua hatua
za kisheria hivyo anatakiwa abadilike sana,” alisema afisa huyo
aliyetambulika kwa jina moja la Janeth.
Mwishoni
mwa wiki iliyopita, kulikuwa na kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa
‘birthday’ ya mtoto wa Nay aliyezaa na mwigizaji wa sinema za Kibongo,
Skyner Ally ‘Skaina’ ambapo mwanamuziki huyo alimtakia heri katika kukua
kwake huku akiweka picha na maneno kwenye kurasa zake za mitandao ya
kijamii.
Hali
ilichafuka baada ya Skaina kuandika waraka mrefu kwenye ukurasa wake wa
Instagram akiambatanisha na picha akiwa na mwanaye na kumtaka Nay
kuacha kumshobokea mwanaye kwani ni miaka mitano sasa hajui anavaa nini,
anakula nini wala anaishi vipi yeye amekalia kuposti picha za mtoto
huyo tu wakati ni baba kwa jina tu.
“Baba
jina anakufanyia promosheni kudanganya Watanzania kama ohoo my twin,
sijui nanunua pisto, hata nguo ya ndani unayovaa hajui thamani yake,
nimevumilia sana miaka mitano sasa nimejisikia kutapika na Mungu
nakuomba unijalie maisha marefu, uwezo, nizidishie riziki, uzima na afya
nikulee mwanangu aje akuone baadaye umekuwa waziri halafu alete pua
yake sijui itakuwaje.
“Mungu
akuweke uje uone mafanikio ya mwanangu, endelea na drama zako ila
tafadhali shobo na mwanangu sitaki, unaposti picha za mtoto wangu za
nini, sitaki shobo na mwanangu, je, wababa wanaojisifu kama wanawapenda
watoto wao halafu hata hawajui mtoto anakula nini, anasoma wapi, anavaa
nini, wapooo….
“Nilikuwa
na dukuduku moyoni ndani ya miaka mitano nimeongea na limetoka ukweli,
unamuweka mtu huru, kutwa kucha kuwadhalilisha wenzio ya kwako
yanakushinda, usiwafunze wenzio, jifunze kwanza kwako,” aliandika
Skaina.
Baada
ya waraka huo, Risasi Mchanganyiko lilimtafuta Nay ili kumsikia
anazungumziaje hilo ambapo alisema hawezi kuzungumza juu ya suala hilo.
“Siwezi kuzungumzia chochote kuhusiana na hilo,” alisema Nay.
Mbali
na Skaina, wiki kadhaa zilizopita msanii wa Bongo Fleva, Faidha Omary
‘Sister Fay’ naye aliibuka na kudai kuzaa na Nay huku akisema kwamba
amemtelekeza, lakini alipoulizwa Nay mwenyewe alikataa katakata kwamba
mtoto huyo siyo wake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)