Thursday, April 27, 2017
Akiri kuua kwa kipigo
Do you like this story?
MAHAKAMA
Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, imeelezwa kuwa mshtakiwa wa
kesi ya mauji, Mwarami Selemani, au Punga, alikiri kumpiga na kumpora
Sh. 850,000 na simu ya mkononi, Wiliam Mkumbo (wakati wa uhai wake)
ambaye baadaye alikufa kutokana na kipigo hicho.
Kadhalika,
mahakama hiyo imeelezwa kuwa mshtakiwa alikiri katika maelezo yake ya
onyo alipohojiwa na polisi katika kituo cha Buguruni miaka tisa
iliyopita.
Madai
hayo yalitolewa jana na shahidi wa nne wa upande wa Jamhuri, Koplo
Ernest (52), mbele ya Jaji Lugano Mwandambo anayesikiliza kesi hiyo.
Upande wa Jamhuri uliongozwa na Mawakili wa Serikali, Anuncitha Leopold na Faraja George.
Akiongozwa
na wakili George, shahidi alidai kuwa Januari 21, 2009, akiwa ofisini
aliitwa na bosi wake aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wakati huo, Camillius
Wambura (kwa sasa Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum ya Dar es Salaam (ZCO).
Alidai
kuwa alipewa jukumu la kumhoji mshtakiwa wa kwanza, Punga kuhusu tukio
la mauaji yaliyotokea eneo la kati ya Sukita na Al Hamza.
Shahidi
alidai kuwa alimpa shahidi haki zake zote za msingi ikiwamo kuita
ndugu, rafiki au wakili wakati akihojiwa na kutoa maelezo yake ya onyo
lakini alikubali kuhojiwa akiwa peke yake.
"Mshtakiwa
aliniambia alisoma Shule ya Msingi Buguruni Moto lakini aliishia darasa
la tano na kujiingiza kwenye matukio ya wizi wa vyombo vya ndani na
nguo.
"Mshtakiwa
alinieleza kuwa mwaka 2001, yeye na rafiki zake, aliowataja kwa majina
moja moja, Chai Jaba, Salum, Chapapa na Kesi, walibadili mtindo wao na
kuanza kupora kwa kutumia silaha ikiwamo nyembe, visu katika kituo cha
daladala Chama Buguruni" alidai shahidi.
Aidha,
shahidi alidai kuwa mshtakiwa alieleza kuwa waliwavizia watu alfajiri
wakati wakienda kazini na waliokuwa wanasafiri na kuwapora vitu
mbalimbali vikiwamo pesa, simu za mkononi na nguo.
"Siku
ya tukio, mshtakiwa akiwa na Chai Jaba, walidamka alfajiri na kujificha
kati ya eneo la Sukita na A Hamza 'tuliona watu watatu mvulana mmoja na
wasichana wawili. Yule kijana alituona akaanza kukimbia, tulimzingira
tukafanikiwa kumkamata.
Tulimpiga
tulimziba matambara ya nguo mdomoni ili asipige kelele alivyotulia
tulimsachi tukafanikiwa kupata Sh. 850,000 na simu moja ya mkononi,”
alinukuu shahidi maelezo ya mshtakiwa.
Akifafanua
zaidi alidai kuwa mshtakiwa alidai kuwa walimwacha kijana yule akiwa
kwenye hali mbaya na kutoweka eneo la tukio na kwamba waligawana fedha
na simu alikwenda kuuza Ilala kwa Chogo.
Kwa
mujibu wa maelezo hayo, baada ya tukio hilo, mshtakiwa alijificha
maeneo ya Kitunda nyumbani kwa wazazi wake na kujihusisha na biashara ya
dawa za kulevya aina ya bangi.
Upande
wa Jamhuri ulifunga ushahidi wao baada ya kuita mashahidi wanne na
vielelezo vitatu ikiwamo ripoti ya daktari na maelezo ya washtakiwa
kukiri kuhusika na mauaji hayo.
Mbali na Punga, mshtakiwa mwingine ni, Rashidi Mbepu maarufu kama China.
Katika
kesi ya msingi, ilidaiwa kuwa Novemba 7, 2008, eneo la Tabata Matumbi,
jijini Dar es Salaam, washtakiwa walimuua William Mkumbo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)