Thursday, April 27, 2017

AUDIO: Wajasiriamali Tandala Makete Kumfuata Diwani wao, Kisa ni Kutimuliwa



Wajasiriamali wanaofanya biashara katika Kijiji cha Tandala Kitongoji cha Posta wilayani Makete, wamepanga kuonana na diwani wa kata yao Mh. Egnatio Mtawa kujadiliana naye agizo linalowataka kuondoa vibanda vyao vya biashara katika eneo hilo

Wakizungumza katika kikao chao kilichofanyika leo asubuhi eneo la stendi ya zamani, wafanyabiashara hao wamesema hawaridhishwi na utaratibu uliotolewa na serikali wa kuwataka waondoke katika eneo wanalofanyia biashara kwa sasa hadi kufikia Ijumaa Aprili 28 mwaka huu

Baadhi yao wamesema kwa sasa wanaendesha maisha yao kwa kutegemea ujasiriamali wao katika kitongoji cha posta ambapo ndipo kwenye wateja wengi, wa kununua bidhaa wanaouza

Mwenyekiti wa wafanyabiashara kata ya Tandala Bw. Elai Mbilinyi amezungumza na Eddy Blog na kuelezea lengo la kikao hicho na dhamira ya wajasiriamali hao kwa sasa kuwa ni kumpelekea diwani ili akawatetee katika Mamlaka za juu

Zaidi sikiliza sauti hii hapa chini>>>>>

0 Responses to “AUDIO: Wajasiriamali Tandala Makete Kumfuata Diwani wao, Kisa ni Kutimuliwa ”

Post a Comment

More to Read