Thursday, April 27, 2017
TRA YAKAMATA MALI ZA LUGUMI
Do you like this story?
Kampuni
ya udalali ya Yono, imefanikiwa kukamata mali za wafanyabiashara wanaodaiwa
kodi ya serikali inayofikia zaidi ya Sh bilioni 68.1. Operesheni ya kukamata
mali hizo kwenye maeneo mbalimbali ndani na nje ya Jiji la Dar es Salaam
imefanywa ndani ya wiki moja.
Katika
operesheni hizo maofisa wa Yono wamekuwa wakishirikiana na maofisa wa Mamlaka
ya Mapato(TRA), ambayo ndiyo imeipa kampuni hiyo kazi ya kukusanya kodi kwenye
maeneo mbalimbali nchini.
Kwa
mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Yono, Scholastica Kevela, Yono
imepewa kazi na TRA kukusanya madeni yake ya kodi kwenye mikoa ya Dar es
Salaam, Pwani Njombe, Mbeya, Iringa na Zanzibar.
Aliwataka
watanzania kuunga mkono jitihada za Rais John Magufuli za kuleta maendeleo kwa
kulipa kodi bila shuruti ili zipatikane fedha za kujenga miundombinu kama
barabara, reli, shule, madaraja, hospitali na zahanati.
Kuhusu
taarifa zilizozagaa kwenye mitandao ya kijamii kwamba hata baadhi ya mali za
Kampuni ya Lugumi zimeshikiliwa, Mkurugenzi huyo alithibitisha kuwa habari hizo
ni za kweli ambapo wanashikilia nyumba za kifahari za mfanyabiashara huyo.
“Mmeniuliza
kwamba mmesikia nyumba za Lugumi zimefungiwa ni kweli, amefungiwa nyumba zake
za kifahari na anadaiwa Sh bilioni 14, yupo mtu anaitwa Gm Dewji naye anadaiwa
Sh bilioni 1.8, Kampuni ya ujenzi ya Mutluhan Construction anadaiwa Sh bilioni
45,” alisema.
Alisema
wanaodaiwa wanapaswa kulipa madeni yao TRA ndani ya siku 14 na kwamba muda huo
ukipita watapewa maelekezo na serikali kama ni kuuza mali hizo ili kufidia
madeni yao.
Ofisa
Mwandamizi wa TRA, ambaye hakupenda jina lake litajwe alithibitisha kwamba
nyumba ya Lugumi iliyoko Upanga mtaa wa Mazengo inashikiliwa na mamlaka hiyo na
ghorofa la kifahari lililoko Mbweni JKT, Dar es Salaam.
“Hakuna
siri maana mkienda kwenye hizo nyumba mtakuta alama ambazo huwa Yono wanaweka
kwa nyumba inayoshikiliwa, nendeni Upanga na kule Mbweni JKT mtakuta hizo
nyumba tunazoshikilia,” alisema
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “TRA YAKAMATA MALI ZA LUGUMI”
Post a Comment