Thursday, April 27, 2017
Hukumu ya Babu Seya na Papii, Mapya Tena Yaibuka
Do you like this story?
Tumaini jipya! Mtoto wa kiume wa mfungwa anayetumikia kifungo cha maisha jela, Nguza Viking ‘Babu Seya’, Mbangu Nguza ameibuka na kusema kuwa, mwaka 2017 ndiyo wa mwisho kwa baba yake na mdogo wake, Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ kuendelea kutumikia kifungo chao cha maisha jela.
Akizungumza katika mahojiano maalum na Amani mwanzoni
mwa wiki hii, Mbangu alisema kuwa, turufu ya mwisho ya hukumu ya ndugu
hao ipo kwenye mikono ya Mahakama ya Haki za Binadamu Afrika (AfCPHR)
yenye makazi yake jijini Arusha ambayo kimsingi vikao vitatu vya awali
vimeshakaa na kubaini kuwa, hukumu ya Babu Seya na Papii ilikuwa na
kasoro.
“Unajua
watu hawafahamu, kule ambako hukumu ya mzee na bwana mdogo (Papii),
ilipelekwa kuna hatua. Kwanza kabisa, wale majaji wanatoka nchi
mbalimbali, kwa hiyo siyo kwamba wanakwenda tu Arusha na kupitia hukumu,
hapana.
“Kilichofanyika
ni kwamba, kuna watu walikaa mara tatu kupitia hukumu ili wajiridhishe
kama kuna makosa ambayo majaji wakikaa watayaona?
“Kwa hiyo vile vikao vimeshakaa mara tatu zote na kubaini kuwa, kweli hukumu ya baba na bwana mdogo ilikuwa ina kasoro.
“Sasa
ndiyo majaji wameitwa ili kupitia na kutoa hukumu yao ya haki. Hii kazi
ingekuwa imeshafanyika muda mrefu ila sasa, kilichotokea ni kwamba,
kuanzia Novemba mwaka jana kama sikosei, watu wa mahakamani walikuwa
likizo ndefu mpaka kwenye Februari mwaka huu, ndiyo wamerudi.
“Kingine
kimechelewesha ni mwaka jana kustaafu kwa rais wa ile mahakama, Jaji
Augustino Ramadhani (kutoka Tanzania), kukawa na kitambo cha kusubiri
kumpata rais mpya, tayari yupo (Sylvain Ore kutoka Cote d’Ivoire).
“Kwa
hiyo bwana, baada ya sasa, wakati wowote ule, majaji watatua Arusha na
kukaa kupitia, naamini, tena narudia kusema, naamini, baba na bwana
mdogo wangu mwaka huu watakuwa huru.
“Hili
suala la wao kuwa huru liko pia kiroho, hata kama mahakama hiyo
isingekaa, bado wale ndugu wangetoka tu, lazima. Kwani Mungu
ninayemtegemea mimi ameshaniambia watatoka,” alisema Mbangu ambaye kwa
sasa ni Mwinjilisti wa Neno la Mungu.
TUMEFIKAJE HAPA?
Nguza
na wanawe watatu walikamatwa Oktoba 12, mwaka 2003 na kufikishwa Kituo
cha Polisi Magomeni, Dar, walipandishwa kizimbani katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu Oktoba 16, mwaka 2003 wakituhumiwa kubaka na
kunajisi watoto 10.
Baada
ya kusikilizwa kesi hiyo Juni 25, 2004, Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar, Addy Lyamuya aliwatia hatiani Babu Seya na
wanaye kwenda jela maisha kwenye Gereza la Ukonga, Dar es Salaam.
Januari
27, mwaka, 2005, Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Thomas
Mihayo alitupilia mbali rufaa yao iliyokuwa ikipinga hukumu.
Awali
mwaka 2004, baada ya kukutwa na hatia katika kesi hiyo, Babu Seya,
Papii Kocha na wakili wao, Mabere Nyaucho Marando walikata rufaa ya pili
ambayo ilitupiliwa mbali.
Mwaka
2010 waliomba tena rufaa ambayo marejeo yake yalisikilizwa na kutolewa
hukumu Februari, 2010. Mahakama iliridhia hukumu ya kifungo cha maisha
kwa Babu Seya na Papii Kocha, ikawaachia huru watoto wake, Mbangu na
Francis Nguza.
Chanzo: Gazeti la Amani
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “Hukumu ya Babu Seya na Papii, Mapya Tena Yaibuka ”
Post a Comment