Thursday, April 27, 2017
Chadema yakanusha kupoke barua ya bunge
Do you like this story?
Chama cha Demokrasia na Maendeleo kimesema kuwa hakijapokea
barua yeyote kutoka bungeni ikiwataka kupeleka majina ya wagombea ubunge
wa Afrika Mashariki (EALA).
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano,
Owen Mwandumbya, amesema kuwa chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema) kinasubiri barua ya maelekezo kutoka bungeni lakini mpaka sasa
hakijapokea.
Aidha, Uchaguzi wa wabunge wa EALA uliingia dosari baada ya wagombea
wa Chadema, Lawrence Masha na Ezekiah Wenje kupigiwa kura za hapana
hivyo kukosa wawakilishi wa nafasi ya ubunge wa Afrika Mashariki.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano, Uenezi na Mambo
ya Nje wa Chadema, John Mrema amesema kuwa mpaka sasa hawajapata barua
kutoka kwa katibu wa bunge Dkt. Thomas Kashililah kuhusu hatua
wanazopaswa kuchukua.
“Tangu umalizike uchaguzi wa awali hatujapata taarifa zozote kutoka
Ofisi ya Bunge, tunasubiri barua kutoka kwa Katibu wa Bunge mchakato
gani ufanyike ili suala hilo lifikie muafaka,”amesema Mrema.
Hata hivyo, Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema kuwa kama Chadema
watapeleka wagombea waliokataliwa basi wategemee majibu yale yale na
kwamba atalazimika kutumia utaratibu mwingine.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “Chadema yakanusha kupoke barua ya bunge”
Post a Comment