Wednesday, December 2, 2015

RAIS WA ZANZIBAR DR SHEIN ATEMBELEA MRADI WA MAJI SAFI NA SALAMA MAKUNDUCHI




Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dr Ali Mohmaed Shein amewataka wananchi kundelea kuwa na imani na serikali yao katika kuwahudumia na kuwawekea mazingira mazuri ya huduma za kijamii.

Dr Shein ametoa kauli hiyo huko Makunduchi mkoa wa kaskazini Unguja wakati akizungumza na wakazi wa Makunduchi baada ya kukagua mradi wa maji safi na salama ambao unasimamiwa na mamlaka ya maji Zanzibar-ZAWA-ambapo amesema serikali itaendelea kuhakikisha ahadi zake kwa wananchi zinatekelezwa huku akiridhishwa na hatua zilizofikiwa za mradi huo ambapo alishuudia visima vitatu na uwekaji wa tangi kubwa la maji.

Mapema mkurugenzi mkuu wa ZAWA-mamlaka ya maji Zanzibar Dr. Mustafa Ali Garu amesema mradi huo umekuwa na mafanikio makubwa na wananchi wa Makunduchi wataanza kufaidika kwa kupata maji safi na salama na kuondokana na kero kubwa ya maji hayo.

Dr Shein amekuwa katika harakati za kutembelea maendeleo ambapo mardi huo wa maji umetokana na nguvu za wananchi na mamlaka ya maji ya Zanzibar na kushirikana na taasisi mbalimbali za kijamii.


0 Responses to “RAIS WA ZANZIBAR DR SHEIN ATEMBELEA MRADI WA MAJI SAFI NA SALAMA MAKUNDUCHI”

Post a Comment

More to Read