Wednesday, December 2, 2015

TANZANIA KURUDISHIWA DOLA ZA KIMAREKANI MILION 6 KUTOKA STANBIC TANZANIA KUPITIA KAMPUNI YA EGMA




Tanzania inatarajia kurudishiwa dola za kimarekani milioni sita sawa na shilingi za kitanzania bilioni 14 zilizotozwa isivyostahili na benki ya Stanbic Tanzania kupitia kampuni ya EGMA.

Fedha hizo zinarejeshwa kwa Tanzania baada ya benki ya Stanbic Tanzania kupitia kampuni ya EGMA kuongeza asilimia moja ya riba baada ya serikali kukopa dola milioni mia sita kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo mwaka 2012 na 2013 na kutakiwa kuzilipa katika kipindi cha miaka 7 kwa riba ya aslimia 1 nukta nne na badala yake ikatozwa asilimia mbili nukta nne ya mkopo wote hali iliyotokana na benki kuu kubaini baadhi ya matatizo.

Kwa mujibu wa Balozi Ombeni Sefue udanganyifu wa utaratibu wa kumtafuta wakala wa ndani yaani Local Agent uliofanywa na benki ya Stanbic Tanzania ulibainika kutokana na uchunguzi uliofanywa na kampuni ya Serious Fraud Office ya London na kufungua kesi ambayo kampuni hiyo ilipata ushindi November 30, 2015 na kuiwezesha Tanzania kurejeshwa fedha hizo huku Balozi Sefue akieleza hatua zinazochukuliwa ndani ya Tanzania kuhusiana na kampuni ya EGMA na benki ya Stanbic Tanzania.

Aidha Balozi Sefue ameishukuru serikali ya uingereza kwa ushirikiano na kuyataka mataifa mengine ya Ulaya kuzisaidia nchi zinazoendelea kupambana na rushwa kutokana na ulaghai unaofanywa na makampuni ya nchi za ulaya badala ya kuzinyooshea vidole kuwa zimeshindwa kupambana na rushwa.


0 Responses to “TANZANIA KURUDISHIWA DOLA ZA KIMAREKANI MILION 6 KUTOKA STANBIC TANZANIA KUPITIA KAMPUNI YA EGMA”

Post a Comment

More to Read