Wednesday, December 2, 2015

SAID BAHANUNZI: TUNAWEZA KUIFUNGA MBEYA CITY, SIFUNGI ILI KUSHINDA UFUNGAJI BORA


Said Bahanuzi (kulia) akiwa katika harakati ya moja ya michezo ya ligi kuu Tanzania bara akiichezea timu ya Mtibwa Sugar


Na Baraka Mbolembole, Dar es Salaam
Mshambulizi wa Mtibwa Sugar FC, Said Bahanunzi anaamini kuwa klabu yake itaishinda Mbeya City FC katika mchezo wa ligi kuu Bara utakaopigwa Desemba 12 katika uwanja wa Sokoine, Mbeya. Mtibwa imeshinda mechi 7 kati ya 9 msimu huu, imejikita katika nafasi ya tatu ya msimamo ikiwa na pointi 22 ( alama 3) nyuma ya vinara wa ligi Azam FC.

“Itakuwa mechi ngumu lakini tayari tulicheza na Mbeya City kabla ya kuanza kwa msimu hivyo hatuna wasiwasi na mechi ijayo. Watakuwa nyumbani lakini kwa namna tunavyoendelea kujifua naamini tunaweza kufanya vizuri na kushinda mechi”, anasema Bahanunzi wakati alipozungumza na mwandishi wa mtandao Jumanne hii.

Akiwa tayari amefunga magoli matatu, mshambulizi huyo aliyechemka Yanga SC imepania kufanya vizuri msimu huu hasa kuisaidia timu yake kumaliza katika nafasi mbili za juu.
“Nahitaji kufunga magoli mengi zaidi kutokana na nafasi yangu lakini sifungi kwa ajili ya kushindania kiatu cha dhahabu bali nahitaji kuisaidia timu yangu kufikia malengo tuliyojiwekea kumaliza katika nafasi mbili za juu”.

0 Responses to “SAID BAHANUNZI: TUNAWEZA KUIFUNGA MBEYA CITY, SIFUNGI ILI KUSHINDA UFUNGAJI BORA”

Post a Comment

More to Read