Wednesday, December 2, 2015

AFRIKA KUSINI YAONGOZA KWA UFISADI AFRIKA


Waafrika wengi wanasema kuwa ufisadi umeongezeka katika kipindi cha miezi 12 na serikali nyingi za bara hilo zikionekana kushindwa kukomesha rushwa na miamala ya siri ya ufisadi.

Hayo yameelezwa na Taasisi ya Transparency International kupitia uchunguzi wake wa maoni.

Katika uchunguzi huo wa maoni, Afrika Kusini imetajwa kuwa nchi inayoongoza kwa ufisadi barani Afrika ikifuatiwa na nchi ya Ghana na Nigeria.


Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini alisema mwezi Oktoba kwamba chama tawala nchini humo kimekuwa kikipoteza uungwaji mkono wa wananchi kabla ya kufanyika uchaguzi wa serikali za mitaa mwakani, kutokana na kuwa chama hicho kimekuwa hakiwachukulii hatua kali mafisadi.


Transparency International imewasilisha uchunguzi huo wa maoni katika kipindi hiki ambapo nchi nyingi za Kiafrika zinakabiliwa na mashinikizo ya wananchi na ya vyama vya upinzani, kufuatia serikali nyingi kushindwa kupambana na ufisadi wa mali ya umma pamoja na kushindwa kuwafungulia mashtaka maafisa wote wa ngazi za serikalini wanaohusika na kashfa za ufisadi.

0 Responses to “ AFRIKA KUSINI YAONGOZA KWA UFISADI AFRIKA ”

Post a Comment

More to Read