Wednesday, December 2, 2015
TAARIFA KUHUSU MAJINA SAHIHI YA WAZIRI MKUU
Do you like this story?
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
WAZIRI MKUU
Kassim Majaliwa (Pichani) anatumia majina matatu kama ifuatavyo: Kassim
Majaliwa Majaliwa au Kassim M. Majaliwa.
Tangu
alipoteuliwa kushika wadhifa huo, kumekuwa na uchanganyaji wa majina yake na
hii ni kwa sababu tangu akiwa chuoni na jeshini, alikuwa akitanguliza kutaja
ubini (jina la ukoo) na ndiyo maana ikawa inasomeka Majaliwa Kassim Majaliwa.
Endapo jina
hilo litaanza kuandikwa na ubini, litapaswa kutenganishwa na koma kama
ifuatavyo: Majaliwa, Kassim Majaliwa.
Waziri Mkuu
Kassim Majaliwa aliteuliwa na Rais, Dkt. John Pombe Magufuli Novemba 19, 2015
na kuthibitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania siku hiyo hiyo.
Aliapishwa Novemba 20, 2015 kwenye Ikulu ndogo ya Chamwino, Dodoma.
IMETOLEWA
NA:
OFISI
YA WAZIRI MKUU,
2
MTAA WA MAGOGONI,
S.
L. P. 3021,
11410
DAR ES SALAAM
JUMATANO,
DESEMBA 2, 2015.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “TAARIFA KUHUSU MAJINA SAHIHI YA WAZIRI MKUU”
Post a Comment