Wednesday, December 2, 2015
MCHAKATO WA KUMPATA MGOMBEA NAFASI YA MEYA JIJI
Do you like this story?
Mwenyekiti wa chadema Wilaya ya Mbeya John Mwambigija wakati wa kikao cha kumpata mgombea Umeya katika Jiji la Mbeya kupitia chama hicho |
Diwani wa kata ya Forest,Henry Mwangambaku ambaye ni moja wapo anaye omba kuwania nafasi yaNaibu Meya jiji la Mbeya kupitia cha cha Chadema. |
JOTO
la kumpata Meya wa Jiji la Mbeya, kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo
Chadema (CHADEMA) limezidi kupanda huku likihatarisha hali ya amani ndani ya
chama hicho ambacho kimeweza kujizolea viti 26 vya udiwani na CCM ikiambulia
viti 10.
Hali
hiyo inatokana na mvutano unaoendelea ndani ya chama hicho unaodaiwa kuchangiwa
na baadhi ya madiwani pamoja na Mbunge wa Jimbo hilo Joseph Mbilinyi.
Wanaowania
nafasi ya Meya wa Jiji la Mbeya ni Albert
Kirato, David Mwashilindi, Lazaro Ngonyani na Fabian Sanga,huku mgombea Albert
Kirato ndio anatajwa kubebwa na Mbunge wa jimbo hilo.
Wakizungumza
na Mtanzania kwa sharti la kutotajwa majina yao, baadhi ya Madiwani, wamekiri
kuwepo kwa mvutano huo na kwamba kama hakutakuwepo na muafaka baina ya pande
mbili hizo madiwani hao wako tayari kumuunga mkono meya kutoka chama cha mapinduzi.
Aidha,
mbali na mvutano huo wa Meya, lakini pia kumekuwepo na mgogoro wa uteuzi wa
viti maalum vya nafasi za udiwani baada ya kudaiwa kufanyika kinyume na
utaratibu huku mbunge huyo akitajwa tena kuwa kinara wa kuwapanga watu wake.
Akizungumza
na Fahari News Mbunge wa jimbo hilo, Joseph Mbilinyi, ambaye alionyesha
kushangazwa na kauli hizo zinazotolewa na baadhi ya madiwani na kudai kuwa yeye
binafsi hana muda wa kuingilia mchakato huo wa kumpata Meya lakini anachoshauri
ni kwamba ni vema kiongozi akapatikana kwa kufuata taratibu na kanuni za chama.
Aidha,
Mbunge huyo aliwataka madiwani hao kutambua kuwa suala la kumpata Meya wa jiji
la Mbeya linapaswa kufuata taratibu na kanuni za chama kwani meya huyo anaenda
kuwawakilisha wananchi wote hivyo wasifanye masihala.
“Ikumbukwe
kuwa umeya wa mbeya mjini si kusimamia machinga wala kuchungulia mipango miji
tunataka meya atakayeenda sambamba na kasi mpya ya Rais John Pombe
Magufui,”amesema.
Aidha,
chama hicho kupitia Jiji la Mbeya, kimefanikiwa kufanya uchaguzi wa uteuzi wa
majina matatu ya nafasi ya Meya kwa kupigiwa kura na madiwani ambapo David
Mwashilindi alipata kura 24, Albert Kirato ambaye alipata kura 8 huku Lazaro
Ngonyani akipata kura 2,.
Hata
hivyo kwa mujibu wa utaratibu wa chama hicho ni kwamba majina hayo
yanawasilishwa makao makuu ya chama ambapo wao ndio wenye dhamana ya kurejesha
jina la Meya.
Mwisho.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MCHAKATO WA KUMPATA MGOMBEA NAFASI YA MEYA JIJI”
Post a Comment