Friday, December 4, 2015

MAN UNITED, BAYERN MUNICH, VITANI KUINASA SAINI YA STAR ANAYEWANYIMA USINGIZI MABEKI




Klabu za Bayern Munich na Manchester United sasa zinapigana vikumbo kutaka kupata saini ya mchezaji raia wa Senegal na klabu ya soka ya Southampton, winga Saidio Mane mwenye miaka 23 katika kuongezea nguvu safu zao za ushambuliaji.

Kocha wa Manchester United, Louis Van Gaal tayari alijaribu kutaka kumsajili winga huyo msimu uliopita kabla ya kukwama na sasa pamoja na usajili wa kinda Anthony Martial, kocha huyo anatafuta kuongeza nguvu safu yake ya ushambuliaji kipindi hiki ambacho nahodha Wayne Rooney akiwa hayuko katika ubora wake uliozoeleka katika soka.

Bayern Munich imekua ni klabu ya mwisho kumtaka mshambuliaji huyo huku Chelsea nao wakiwa miongoni mwa timu zinazomtolea macho winga huyo anayekuja juu na kuteka hisia za wanamichezo wengi hivi sasa huku akiwa amefunga magoli 17 tangu atue Southampton mwaka jana.

Kocha Louis Van Gaal akihojiwa katika hafla ya shirika la watoto duniani UNICEF, alimtaja Mane kama miongoni mwa vipaji vikubwa hivi sasa katika soka na sasa atajaribu kumsajili mchezaji huyo mwezi January katika dirisha dogo la usajili.

0 Responses to “MAN UNITED, BAYERN MUNICH, VITANI KUINASA SAINI YA STAR ANAYEWANYIMA USINGIZI MABEKI”

Post a Comment

More to Read