Friday, December 4, 2015
UPOTEVU WA MAKONTENA 329, MAOFISA WANNE TRA WAPANDISHWA KIZIMBANI
Do you like this story?
Watuhumiwa wa kesi hiyo wakiingia ndani ya gari. |
Hapa Masamaki na wenzake wakiingia ndani ya gari kuelekea gereza la Segerea. |
Gari la polisi lililowabeba watuhumiwa hao likiondoka mahakamani hapo. |
Na
Dotto Mwaibale
KASI
ya utendaji kazi wa Rais Dk.John Pombe Magufuli na Waziri Mkuu Majaliwa Kasim
Majaliwa imeanza kuwagusa baadhi ya watendaji wa Serikali baada ya maofisa
wanane wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), akiwemo Kamishna wa Forodha
wa mamlaka hiyo Tiagi Masamaki (56) kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za kutoa
makontena 329 bandarini bila ya kulipiwa kodi na kuisababishia Serikali hasara
ya sh. bilioni 12.7 za kitanzania.
Ukimuondoa
Masamaki maofisa wengine waliopandishwa kortini ni Habibu Mponezya (45) Meneja
wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja,Bulton Mponezya (51)
Wakili
wa Serikali Mwandamizi Christopher Msigwa akisaidiana na Peter Vitalis
ameadi leo mchana mbele ya Hakimu Mkazi Huruma Shahidi wa Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kuwa watuhumiwa hao wanatuhumiwa kwa makosa
mawili.
Alidai
makosa mawili ya uhujumu uchumi ni kula njama ya kuidanganya Serikali na
kuisababishia Serikali hasara. Kesi hiyo ni namba 35/2015 ya uhujumu uchumi.
Ilidaiwa
katika shtaka la kwanza katika tarehe tofauti kati ya Juni 1 na Novemba 17
mwaka huu, sehemu isiyojulikana ndani ya Jiji la Dar es Salaam kwa pamoja
walikula njama ya kuidanganya Serikali kuwa sh. bilioni 12.7 zimetolewa
kwa kutoa makontena 329 katika Bandari Kavu ya Azam, baada ya kodi zote
kutolewa.
Katika
shtaka la pili, washtakiwa wanatuhumiwa katika ya Juni Mosi na Novemba 17 mwaka
huu ndani ya Jiji la Dar es Salaam walishindwa kutimiza majukumu yao kwa namna
inavyotakiwa na kusababisha Serikali kupata hasara ya sh. bilioni 12.7.
Baada
ya washtakiwa hao kusomewa makosa yao, Hakimu Shahidi aliwaeleza kuwa mahakama
hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo, kwa hiyo hawatakiwi kujibu chochote
kama kweli au si kweli.
Aliongeza
kuwa Mahakama Kuu ndiyo inamamlaka ya kusikiliza kesi hiyo, kwa hiyo kama
wanataka dhamana wapeleke maombi ya dhamana katika mahakama hiyo.
“Kama
mnataka dhamana pelekeni maombi Mahakama Kuu kwa sababu mahakama hii hawezi
kutoa dhamana,” alisema Hakimu Shahidi
Hata
hivyo, upande wa utetezi ulidai kuwa kesi hiyo ifikishwa mahakamani hapo bila
kibali na pia waliomba mshtakiwa namba nne Mrema anamtoto mchanga kwa hiyo
wanaiomba mahakama imfikirie.
Wakili
Msigwa alidai upelelezi bado unaendelea, wanaomba tarehe nyingine ya kutajwa.
Kesi hiyo itatajwa Desemba 17 mwaka huu kuangalia kama upelelezi utakuwa
umekamilika.
(Imeandaliwa
na mtandao wa habari za jamii)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ UPOTEVU WA MAKONTENA 329, MAOFISA WANNE TRA WAPANDISHWA KIZIMBANI”
Post a Comment