Wednesday, June 25, 2014
JAMBAZI ALIYETOKA JELA KWA MSAMAHA WA RAIS ADAIWA KUFANYA MAUAJI KWA KUMNYONGA MTU GONGO LA MBOTO
Do you like this story?
Mtu mmoja anayedhaniwa kuwa ni jambazi
anatafutwa na jeshi la polisi kwa madai ya kufanya matukio mbalimbali ya
kiharifu likiwemo tukio la hivi karibu kumnyonga hadi kufa dada mmoja
aliyetajwa kwa jina la Bahati Husein mkazi wa Ulongoni A Gongo la Mboto jijini
Dar es Salaam.
Akizungunza , dada wa marehemu
aliyejitambulisha kwa jina la Moshi Hussein alisema mtu huyo ambaye
anatambulika kwa jina moja la Godfrey, kabla ya kumuua dada yake alikuwa
akimtamkia mara kwa mara kwamba ipo siku atamuua.
“Tulikuwa tunaona kama utani maana
alikuwa akisema suala la kumuua mara kwa mara na siku chache kabla ya kumuua
walikuwa na ugomvi ambapo Godfrey alikuwa akimhisi dada yangu (ambaye kwa sasa
ni marehemu) anamahusiana na mwanaume mwingine hali iliyosababisha kaka aje na
kuwasuruhisha,” anaeleza Moshi huku akilia kwa uchungu.
Aliendelea kusema baada ya kusuruhishwa
alionekana kuridhika na kumtaka mkewe (marehemu) ampikie ugali ambapo marehemu
alifanya kama alivyoagizwa lakini usiku wake akambyonga hadi kufa.
“Baada ya kumuua aliondoka usiku huo
huo na asubuhi alipiga simu kwa ndugu akisema eti anataka kuongea na mkewe kwa
hiyo mtu aende ampe simu ili wazungumze wakati anajua nini amekifanya!”
anasimulia Moshi.
Alipoulizwa wao walijuaje kama marehemu
alinyongwa hadi kufa, Moshi alisema baada ya kifo hicho walikwenda kuripoti
kituo cha polisi Stakishali ambapo kabla ya kujua kama ndugu yao ni marehemu
walimchukuwa na kumkimbiza katika Hospitali ya Amana ambapo mara baada ya
madaktari kumchukuwa vipimo iligundulika kuwa dada tayari alikuwa mfu.
“Tulipohoji chanzo cha kifo chake ndipo
tulipoambiwa kwamba vipimo vinaonyesha marehemu amenyongwa na shingo yake
imevunjika mara mbili,” alisema.
Aidha, akitoa historia ya mtu huyo
anayetajwa kama jambazi sugu, kaka wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina la
Abdallah Husein, alisema kabla ya kutokea kwa tukio hilo Godfrey alikuwa
akitumikia kifungo cha miaka 20 jela kwa kosa kama hilo (la mauaji) na
aliachiwa huru mwaka jana kwa msahama wa rais.
“Hadi anakuja na kuishi na dada yetu
bwana huyu alikuwa jela akitumika miaka 20 kwa kosa kama hili. Kwa sababu huyu
jamaa (Godfrey) ni mtu mwenye wivu sana na chanzo cha kufungwa miaka 20 ilikuwa
ni baada ya kumfumania mkewe na mwanaume mwingine gesti ambapo aliwauawa wote
na kesi kwenda mahakamani na kukutwa na hatia na kufungwa miaka hiyo 20 leo
kamuua dada yangu, ina niuma sana,” alisema Abdallah.
Aidha, mjumbe wa eneo hilo la Ulongoni
A ambaye jina lake hakulikuweza kupatikana mara moja alithibitisha kutokea
tukio hilo.
Jitihada za kumpata Kamanda wa polisi
mkoa wa Kipolisi Ilala, Kamanda Mariathe Minangi hazikuzaa matunda baada ya
simu yake kupokelewa na mtu aliyejitambulisha ni mlinzi wake na kudai RPC yupo
kikaoni. Jitihada za kumtafuta RPC bado zingaliendelea kwa ajili ya kutolea
ufafanuzi tukuio hili.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “JAMBAZI ALIYETOKA JELA KWA MSAMAHA WA RAIS ADAIWA KUFANYA MAUAJI KWA KUMNYONGA MTU GONGO LA MBOTO ”
Post a Comment