Wednesday, June 25, 2014

MARCIO MAXIMO ASAINI MKATABA NA YANGA.



KOCHA Mkuu wa zamani wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars Mbrazil,  Marcio Maximo anatarajia kuwasili nchini leo mchana akitokea kwao kwa ajili ya kuinoa timu ya soka ya Yanga iliyoanza mazoezi jana.

kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Manyara Sports Management, Ally Mleh Maximo anawasili sambamba na msaidizi wake Leonardo Neiva.
Ni kweli kocha Marcio Maximo amekubali kuingia mkataba na timu ya
Yanga ambapo anatarajiwa kuanza kazi rasmi tarehe 27/06/2014 ambapo
atafuatana na msaidizi wake Leonardo Neiva. Mazungumzo ya makubaliano
hayo yalichukua muda mrefu kidogo hatimaye tumefikia
makubaliano.Tunashukuru mungu kila kitu kimekamilika,” alisema Mleh.

Mleh alisema Manyara sports Management ni kampuni inayojishughulisha na uwakala wa
wachezaji na makocha, kutafuta wadhamini katika michezo, na usambazaji
wa vifaa vya michezo.
Alisema kwa niaba ya Marcio Maximo anapenda kuushukuru uongozi wa klabu ya
Yanga, kwa kweli wameonyesha  umakini na professional kwa muda wote wa
majadiliano. Nawaomba wachezaji,wanachama na wapenzi wote wa Yanga
wampe ushirikiano.
Baada ya kumaliza mkataba wake wa kuifundisha Taifa Stars nchini
aliingia mkataba na timu kubwa nchini Brazil  mpaka mkataba wake
ulipoisha.Kwa wakati huu kulikuwa na mazungumzo na timu mbalimbali
Zilizotoa  ofa nchini China, Ethiopia na Afrika kusini lakini Yanga
wamefanikiwa kumnasa kocha huyo.

0 Responses to “MARCIO MAXIMO ASAINI MKATABA NA YANGA.”

Post a Comment

More to Read