Saturday, June 21, 2014
MAONI YA MH. GODBLESS LEMA ALIYOYATOA BUNGENI NA KUACHA GUMZO HAYA HAPA.
Do you like this story?
June 20 2014 Mbunge wa Arusha mjini
Godbless Lema ni miongoni mwa waliowasha vipaza sauti kwenye bunge la bajeti
linaloendelea Dodoma ambapo sehemu ya alichochangia ni hiki kinachofata hapa
chini.
‘Dola bilioni moja miaka kumi nyuma
ilikua ni Trilioni 11 lakini sasa unaongelea Trilioni 17 kwa hiyo shilingi
imeshuka thamani lakini unashangaa kwanini tunaendelea kuongeza ushuru kwenye
pombe na sigara kama chanzo cha mapato ya taifa letu, nchi nyingi duniani
zinazoongeza ushuru kwenye pombe na sigara lengo lake ni kuona idadi ya
wanaokunywa na kuvuta inapungua tofauti na Tanzania ambako lengo limekua ni
kukusanya mapato, hiki ni kitu cha kusikitisha sana’
‘Nimekwenda Singida hivi karibuni
kwenye ziara ya chama chetu na Mh. Tundu Lissu, ukiwa Singida na Dodoma unaona
kuna jua kali… Singida Same serikali imeweka vikao barabarani >> NENDA
POLEPOLE HAPA KUNA UPEPO MKALI UNAUA << ingekua ni taifa kama Israel,
upepo mkali hauwekewi vibao vya kuua bali upepo mkali unachukuliwa kuwa umeme’
‘Sehemu kubwa ya Singida na Dodoma ni
semi desert, serikali ingeweza kabisakabisa kutengeneza solar village maeneo
haya ikatengeneza umeme mkubwa kupitia nguvu za jua ukaingiza kwenye gridi ya
taifa na mngeweza kupunguza bili za umeme ambazo Wananchi kwa sasa wanapigwa
huko mitaani’
‘Hata kama kutakua na mpango wa aina
gani, unapokua na serikali ambayo haifikirii kwa upana… serikali ambayo inasema
bado inakopesheka, bado tunaweza kukopesheka…. mimi ningekua ni nyinyi,
ningekwenda kukopa barabara zote nchi nzima zijengwe, ningeenda kukopa reli
ijengwe, ningekwenda kukopa Airport ziboreshwe na ningekwenda kukopa serikali
yenu ihamie hapa Dodoma’
‘Watu wengi wamesema kuhusu serikali
kuhamia hapa Dodoma, ukiondoa serikali Dar es salaam ukaileta Dodoma utaipa
nguvu hii Ruaha ambayo hakuna watalii, watalii wataanza kwenda kwa sababu wakuu
wote wa nchi watakuwa wanakuja Dodoma kufanya mikakati yao kwa hiyo centre ya
mapumziko itakua ni Iringa, Mbeya na Singida hapa’
‘Mimi ningekua nyinyi ningefanya
maamuzi magumu, ningechukua Mawaziri wote na makatibu wakuu wote waje hapa
wakae gesti na wengine wakae kwenye matent kwa sababu msipochukua maamuzi
serious hamuwezi kuibadili hii nchi, hii nchi haitobadilishwa kwa Kinana
kuzunguka kutafuta kura za Urais huko kote anakokwenda’
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MAONI YA MH. GODBLESS LEMA ALIYOYATOA BUNGENI NA KUACHA GUMZO HAYA HAPA.”
Post a Comment