Monday, June 30, 2014
MECK SADIQ NA KABWE WAUNGWA MKONO DAR.
Do you like this story?
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiq. |
Mkurugenzi wa Jiji Wilson Kabwe.
|
Baadhi ya wakazi wa
jiji la Dar es Salaam wamemuunga mkono Mkuu wa Mkoa Saidi Meck Sadiq, na
Mkurugenzi wa Jiji Wilson Kabwe kwa hatua walizochukua dhidi ya wamachinga.
Kufuatia uungwaji
mkono wakaazi hao wamemtaka Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan Zungu (CCM), kuacha
kuwatetea wafanyabiashara wadogo (Wamachinga), wanaofanya biashara katika
maeneo ya siyo rasmi.
Hivi karibuni Mbunge
huyo, akiwa bungeni alikaririwa na vyombo vya habari akiwashutumu Mkuu wa Mkoa
wa Dar es Salaam, Said Meck Sadik na Mkurugenzi wa Jiji, Wilson Kabwe, kuwa
wamekuwa wakilivuruga jiji hilo kwa kuwakamata Wamachinga.
Wakizungumza kwa
nyakati tofauti na jijini wakazi hao, walisema ni jambo la kushangaza, baadala
ya mbunge kusimama kidete kwa kupigania sheria baadala yake anaungana na
kuwatetea watu wanaovunja sheria.
Walisema wanamuunga
mkono mkuu wa mkoa na Mkurugenzi wa Jiji kwa sababu baada ya kubaini kazi
yao imeleta tija kwani mitaa mingi ya Kariakoo imekuwa safi pia msongamano wa
magri na watu umepungua.
Kitwana Seif, ambaye ni
mkazi wa Kinyerezi, alisema ukiona kiongozi yeyote anatetea watu wanaovunja
sheria basi hiyo ni ishara tosha kuwa ameshindwa majukumu yake na hana uhakika
wakuendelea na kazi anayoifanya.
Alishangaa kumsikia
Zungu akitamka maneno haya “Sadik na Kabwe hawafai hata kidogo, wanachokifanya
pale Dar es Salaam ni hatari kwetu maana wanawaondoa wapiga kura wa katiba mpya
na wa uchaguzi mkuu, wakiachwa waendelee na utaratibu wao tusidhani kama
tutapata kura,” alinukuu kauli.
Kwa upanade wake
Mwanaharakati wa Mazingira Amos Joseph, alisema, haingii akilini kwa mbunge
huyo kuwatetea watu wanaovunja sheria eti kwa kisingizio cha kuwa ni wapiga
kura wake.
“Wamachinga ni tatizo
jijini Dar es Salaam kwa sababu wanachangia msongamano wa magari pia kufanya
watembea kwa miguu kukosa uhuru kwasababu wanafanya biashara hata kwenye maeneo
ya hifadhi ya barabara ambako wakati mwingine ni maeneo ya watembea kwa
miguu,”alisema Joseph.
Alitoa wito kwa Mkuu
wa Mkoa na Mkurugenzi wa jiji kuwa waendelee na kazi hiyo nzuri ya kuwadhibiti
Wamachinga huku wakimpuuza mbunge huyo ambaye hajui wajibu wake.
Mmoja wa Watendaji
wa Manispaa moja jijini, alisema sio kweli kama wanapinga utaratibu
unaondelea wa kuwaondoa wamachinga kwani hata wao walikuwa hawapendezwi na
uwepo wafanyabiashara hao katika maeneo yasio rasmi.
Alisema kama ingekuwa
sio wanasiasa kuingilia kati majukumu yao anahakika kwa kushirikiana na askari
mgambo wangefanikiwa kuwazuia kwenye maeneo hayo tangu awali.
Zungu alitoa shutuma
hizo juzi bungeni alipokuwa akichangia mjadala wa bajeti ya serikali ya mwaka
2014/2015 ambapo alisema viongozi hao wawili wametangaza vita dhidi ya
wamachinga, mama na baba lishe kwa kupora bidhaa zao na kuwavunjia maeneo
wanayofanyia shughuli zao za kujipatia kipato.
“Sadik na Kabwe
hawafai hata kidogo, wanachokifanya pale Dar es Salaam ni hatari kwetu maana
wanaowaondoa wapiga kura wa katiba mpya na wa uchaguzi mkuu, wakiachwa
waendelee na utaratibu wao tusidhani tutapata kura,” alisema.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MECK SADIQ NA KABWE WAUNGWA MKONO DAR.”
Post a Comment