Monday, June 23, 2014
SEKRETARIETI YA AJIRA YAZIPA RUNGU SERIKALI ZA MITAA
Do you like this story?
Serikali za mitaa zitaruhusiwa kuanza
kuajiri watumishi wa baadhi ya kada za chini katika mwaka wa fedha wa
2014/2015.
Akihojiwa katika Maonyesho ya Wiki ya
Utumishi wa Umma kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam, Msemaji wa
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Riziki
Abraham, alithibitisha kuwa Sekretarieti hiyo itakasimu sehemu ya madaraka yake
ya kuendesha mchakato wa jira serikalini kwa serikali za mitaa.
“Sekretarieti ya Ajira imeandaa mpango
wa kukasimisha madaraka yake ya kuendesha mchakato wa ajira serikalini kwa
baadhi ya kada za chini (operation staff) kwenye mamlaka za Serikali za Mitaa
na mchakato huo utaanza mwaka wa fedha 2014/15” alisema.
Pia, alisema katika kila nafasi ya kazi
inayotangazwa kwa waombaji, Sekretarieti hiyo haizingatii GPA (kiwango cha
ufaulu kwa masomo yote ). Alieleza kuwa zipo kada, ambazo GPA inazingatiwa ;na
zipo kada ambazo kinachoangaliwa ni ufaulu tu wa kawaida na sifa
zilizoainishwa.
“Zipo baadhi ya kada ambazo masharti
yake ni pamoja na kuwa na GPA ya kiwango fulani. Kada ambazo ni lazima GPA
kuangaliwa ni kama vile kada za wakufunzi wa vyuo mbalimbali. Kazi nyingine
hazina masharti ya GPA, kinachoangaliwa ni ufaulu tu na sifa zilizoainishwa
katika tangazo la nafasi za kazi kulingana na kada husika”, alisema Riziki.
Alitaja moja ya matatizo wanayopata
waombaji wa kazi kuwa ni kupotelewa na vyeti vya kitaaluma. Alisema waombaji wa
kazi ambao wamepata tatizo hilo, wanachopaswa kufanya ni kuripoti kwenye
mamlaka husika, alikokuwa amepata cheti hicho ili apewe mwongozo wa kufanya na
kutangaza kupotelewa kwa cheti au vyeti kwenye chombo cha habari
(gazeti).
“Ikithibitika hivyo mamlaka husika kwa
mfano Baraza la Mitihani wana utaratibu wa kuwasiliana na Sekretarieti ya Ajira
kwa kutoa majina ya watu waliopoteza vyeti na hatimaye huruhusiwa kufanya
usaili” alisema.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “SEKRETARIETI YA AJIRA YAZIPA RUNGU SERIKALI ZA MITAA ”
Post a Comment