Sunday, June 29, 2014

USAJILI VITAMBULISHO VYA TAIFA WAINGIA PWANI.



Mamlaka ya Vitambulisho imezindua zoezi la utambuzi na usajili katika mkoa wa Pwani tarehe 28/06/2014 na zoezi hilo linaanza rasmi Julai Mosi,2014.

Akizindua zoezi hilo, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza aliwasisitiza Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi Watendaji wa Halmshauri na Watendaji wote katika mkoa huo kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika zoezi hilo.

Aidha, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dickson Maimu aliwaomba wakazi wa Pwani wenye umri wa miaka 18 na zaidi kujitokeza kwa wingi kwenye zoezi hilo kwa kufika kwenye vituo vya usajili wakiwa na nyaraka zinazothibitisha uraia, umri na makazi yao ambazo ni cheti cha kuzaliwa, kitambulisho

cha mpigakura, pasi ya kusafiria, leseni ya udereva, vyeti vya elimu, kadi ya bima ya afya na kadi ya mlipakodi.
Vituo vya usajili vitafunguliwa saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 11:00 jioni. Zoezi hili ni bure hivyo wananchi wasirubuniwe na watu wanaotaka kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu. 

0 Responses to “USAJILI VITAMBULISHO VYA TAIFA WAINGIA PWANI.”

Post a Comment

More to Read