Tuesday, June 24, 2014
VIGOGO 12 WA BIASHARA HARAMU YA MADAWA YA KULEVYA NCHINI WAFIKISHWA MAHAKAMANI.
Do you like this story?
Mkurugenzi wa vipimo wa tume hiyo, Gloria Omari
|
|
Hatua ya serikali kuamua kupambana na Uingizwaji wa
Biashara haramu ya Madwa ya Kulevya tayari hatua hiyo imeanza kuzaa matunda
ambapo jumla ya Vigogo 12 wa biashara hiyo nchini wamekamatwa na
kesi zao zipo mahakamani.
Tarifa hiyo imebainishwa na Mchambuzi Mkuu wa Tume ya
Kuratibu Udhibiti wa Dawa za Kulevya nchini, Januari Ntisi, mjini Mbeya katika
mkutano na Waandishi wa Habari kuhusu maadhimisho ya Kitaifa ya kupinga
matumizi ya dawa za kulevya yatakayofanyika mkoani hapa ambapo mgeni rasmi anatarajiwa
kuwa Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilali, anayewasili (Juni 25) mjini
hapa kwa ajili ya maadhimisho hayo.
Ntisi amesema vigogo hao 12 ni baadhi ya wafanyabiashara
wakubwa wa biashara hiyo ambao pia wanatafutwa kimataifa na tayari hatua za
kisheria zimeshaanza kuchukuliwa kwa kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo.
Hata hivyo, Ntisi hakuwa tayari kutaja majina ya vigogo hao
kwa madai ya sababu za kiusalama ingawa alidai tayari kesi zao zipo mahakamani.
Hata hivyo, tume hiyo imekiri kuwa bado biashara ya dawa za
kulevya nchini ni changamoto kubwa katika mustakabali wa taifa hivyo Ntisi
alisema ni suala linalohitaji nguvu ya watanzania wote ili kukabiliana na jambo
hilo.
Kuhusu hofu ya wananchi kuwa kuna uchakachuaji wa dawa za kulevya
zinazokamatwa ambazo ama huonekana kuwa si dawa halisi au hupotea katika
mazingira yasiyoeleweka, Mkurugenzi wa vipimo wa tume hiyo, Gloria Omari,
alisema hakuna uchakachuaji unaofanywa bali matokeo yanayotangazwa yanatokana
na vipimo halisi kwa dawa husika.
Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, aliwataka wananchi wa mkoani
hapa kuwataja viongozi wa Serikali wanaojihusisha na biashara ya dawa za
kulevya ili kuiwezesha Serikali kukabiliana na mtandao wa wahusika wa dawa
hizo.
Kwa mujibu wa takwimu hizo, jumla ya
dawa hizo za kulevya zenye thamani ya shilingi bilioni 30 zilikamatwa, ambapo
heroini zilikamatwa kilo 742.5, kokeini kilo 348.3, bangi kilo 77,740, huku
mirungi ikikamtwa kilo 16,334.
Huku zikionyesha kuwa tangu
mwaka 2010 hadi kufikia machi 2013, jumla ya vijana 20,000 walikuwa wanaendelea
na matibabu katika vituo mbalimbali baada ya kuathiriwa na dawa
hizo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “VIGOGO 12 WA BIASHARA HARAMU YA MADAWA YA KULEVYA NCHINI WAFIKISHWA MAHAKAMANI.”
Post a Comment