Tuesday, June 24, 2014
MWANAMKE ALIYE ACHIWA HURU NCHINI SUDANI AKAMATWA TENA.
Do you like this story?
Taarifa kutoka nchini Sudan zinasema kuwa
mwanamke aliyeachiliwa hapo jana kwa kosa la kuasi dini amekamatwa tena.
Mwanamke huyo Meriam Ibrahim, alikuwa amehukumiwa kifo kwa kosa la
kuolewa na mwanamume mkristo na kukana dini ya kiisilamu alikamatwa akiwa na
familia yake katika uwanja wa ndege mjini Khartoum.
Watu waliomkata walikuwa wamevalia mavazi ya kiraia ingawa wanaaminika
kuwa wanajeshi wa serikali.
Duru zinasema kuwa Meriam Ibrahim aliyejifungulia jela alikuwa
anajiandaa kuondoka nchini Sudan pamoja na familia yake.
Haijulikani kwa nini alikamatwa na karibu watu arobaini waliokuwa
wamavalia mavazi ya kiraia siku moja tu baada ya kuachiliwa kuambatana na
uamuzi wa mahakama ya rufaa.
Meriam alikamatwa kwa mara ya kwanza mwezi Februari na kujifungulia
mtoto wake msichana jela baada ya kuhukumiwa.
Alikamatwa mara ya kwanza mwezi Februari na kujifungulia mtoto wake
msichana jela punde baada ya kuhukumiwa.
Familia yake imepelekwa katika makao makuu ya idara ya ujasusi.
Kabla ya kuzuiliwa kwaketena, jamii ya kimataifa yalipongeza uamuzi wa
kuachiliwa kwake na kumuondolea hukumu ya kifo chake.
Via>bbc
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MWANAMKE ALIYE ACHIWA HURU NCHINI SUDANI AKAMATWA TENA.”
Post a Comment