Tuesday, June 24, 2014
24 Jun 2014 HAWA NDIYO WACHEZAJI 11 WA YANGA AMBAO HAWATAICHEZEA TENA TIMU HIYO MSIMU UJAO
Do you like this story?
Ikiwa dirisha la usajili
limeshafunguliwa tangu wiki iliyopita kwa timu mbali mbali kuanza kufanya
usajili wa wachezaji na zingine zikianza mazoezi, timu ya Young Africans
imeweza kuweka wazi majina ya awali ya baadhi ya wachezaji ambao hawataitumikia
katika msimu ujao wa 2014/2015.
Young Africans ambayo msimu uliopita
ilikua na kikosi bora kabisa ambacho kiliweza kuwatoa jasho Mabingwa wa
Kihistoria Barani Afrika timu ya Natioal Al Ahly katika mashindano ya Klabu
Bingwa Afrika, ambapo Mabingwa hao wa kutoka nchini Misri waliweza kusonga
mbele kwa mikwaju ya penati.
Msimu uliopita Young Africans ilikuwa
na kikosi cha wachezaji 30 kutoka timu ya Wakubwa na wachezaji watano (5)
kutoka timu ya vijana (U20) waliokuwa wamepandishwa kwa ajili kupata
uzoefu na kuingozea nguvu timu ya wakubwa katika michezo mbalimbali.
Kutokana na ripoti ya Benchi la Ufundi
iliyowasilishwa mara baada ya kumalizika kwa Msimu wa Ligi Kuu 2013/2014 baadhi
ya wachezaji hawataitumikia tena Yanga SC kwenye msimu ujao, wachezaji 11
wamemaliza muda wao na kumalizana na uongozi hivyo wapo huru kujiunga vilabu
mbalimbali:
Wachezaji hao ni:
1. David Luhende
2. Athuman Idd "Chuji"
3. Geroge Banda -U20
4. Yusuph Abdul -U20
5. Rehani Kibingu -U20
6. Hamisi Thabiti
7. Reliants Lusajo
8. Bakari Masoud - U20
9. Shaban Kondo
10. Abdalllah Mguhi "Messi"
U-20
11. Ibrahim Job
Hii ni orodha ya awali ya wachezaji
ambao hawataitumikia Yanga SC msimu ujao, huku zoezi la usajili likiendelea
kujaza baadhi ya nafasi zilizopo kulingana na maelekezo ya Benchi la Ufundi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ 24 Jun 2014 HAWA NDIYO WACHEZAJI 11 WA YANGA AMBAO HAWATAICHEZEA TENA TIMU HIYO MSIMU UJAO”
Post a Comment