Wednesday, December 23, 2015
RAIS DK. JOHN POMBE MAGUFULI AFANYA UTEUZI WA MAWAZIRI KUJAZA NAFASI ZILIZOKUWA WAZI
Do you like this story?
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemalizia kujaza nafasi za
uteuzi wa Mawaziri na Naibu Waziri alizobakiza wakati akitangaza baraza la
Mawaziri la kwanza katika awamu ya tano yautawala wake
Uteuzi
huo ni kama ifuatavyo;
1.Profesa Jumanne
Maghembe -Ameteuliwa kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii.
2.Dkt. Philip
Mpango – Ameteuliwa kuwa Waziri wa Fedha na Mipango (Ni baada ya kumteua kuwa
Mbunge).
3.Mhandisi
Gerson Lwenge – Ameteuliwa kuwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji.
4.Dkt. Joyce
Ndalichako – Ameteuliwa kuwa Waziri wa Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi.(Ni
baada ya kumteua kuwa Mbunge)
5.Mheshimiwa
Hamad Masauni – Ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
6.Prof.Makame
Mbarawa –Amehamishwa kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji na kwenda Wizara ya
Ujenzi, uchukuzi na Mawasiliano
Katika hatua
nyingine Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
amewatakia heri watanzania wote katika Sikukuu za Maulid, Christmas na Mwaka
Mpya na kuwataka washerehekee kwa amani na utulivu.
Gerson Msigwa
Kaimu
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
23 Desemba,
2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
.gif)


0 Responses to “RAIS DK. JOHN POMBE MAGUFULI AFANYA UTEUZI WA MAWAZIRI KUJAZA NAFASI ZILIZOKUWA WAZI”
Post a Comment