Wednesday, December 23, 2015
WAZIRI AFUTA SEMINA KWA MADIWANI NCHINI
Do you like this story?
Serikali
imesema mafunzo kwa ajili ya madiwani wote hayatakuwepo na badala yake
wenyeviti na makamu wa wenyeviti kote nchini ndio watapatiwa mafunzo ya namna
ya kusimamia halmashauri zao.
Naibu Waziri,
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) anayeshughulikia
Utumishi na Utawala Bora, Selemani Jafo alisema hayo wakati alipofanya ziara ya
kutembelea Chuo cha Serikali za Mitaa cha Hombolo mjini Dodoma.
“Madiwani
ni wengi wote kuwapatia mafunzo haiwezekani kila halmashauri itatoa mwenyekiti
na makamu mwenyekiti, meya na naibu meya” alisema
Jafo.
Alisema mafunzo
hayo yatahusisha wenyeviti wa halmashauri na makamu wao kutoka halmashauri 185
nchini na kuwaagiza wakurugenzi kuhakikisha viongozi hao wanafika Chuo cha
Hombolo tayari kwa ajili kwa mafunzo hayo.
Alisema miaka
ya nyuma kulikuwa na utaratibu wa kuwapatia mafunzo madiwani waliochaguliwa
baada ya Uchaguzi Mkuu, lakini sasa ni wenyeviti na makamu wenyeviti wa
halmashauri ndio watapatiwa mafunzo hayo.
Alisema
halmashauri 185 zilizopo nchini zitapeleka watu wawili kila halmashauri na
waliopata mafunzo hayo watakwenda kuwafundisha wengine.
Naibu Waziri
alisema kulikuwa na changamoto nyingi katika Uchaguzi Mkuu uliopita na madiwani
walichaguliwa kutokana na sifa zao na wengine wananchi walifanya uchaguzi wa hasira,
lakini mwisho wa siku kiongozi aliyetakiwa alipatikana.
Alisema
madiwani wapya waliopatikana wapo wafanyabiashara, wanafunzi na watu wa kada
mbalimbali ambao wote walitakiwa kufundishwa namna ya kutenda kazi zao.
Hata hivyo,
alisema mafunzo kwa ajili ya madiwani wote hayatawezekana, bali viongozi wa
madiwani hao ndio watapatiwa mafunzo hayo.
Kwa upande
wake, Mkuu wa Chuo cha Serikali za Mitaa, Dk Emmanuel Gibai alisema maandalizi
kwa ajili ya mafunzo hayo yamekamilika.
Awali yalipangwa
kutolewa kwa madiwani wote, lakini kutokana na maelekezo hayo wahusika
watakaotakiwa kupatiwa mafunzo hayo watayapata.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
.gif)


0 Responses to “ WAZIRI AFUTA SEMINA KWA MADIWANI NCHINI”
Post a Comment