Thursday, December 24, 2015
POLISI WAUANA KWA RISASI JIJINI MWANZA WAKIWA LINDONI
Do you like this story?
![]() |
| Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, SACP Justus Kamugisha. |
ASKARI Polisi
wa Kituo cha Polisi Nyamagana jijini Mwanza, Konstebo Daud Masunga Elisha,
amemuua askari mwenzake, Konstebo Petro Saimon Matiko kwa risasi na baadaye na
yeye kujiua kwa risasi.
Tukio hilo
lilitokea jana saa 8.30 mchana jijini Mwanza katika eneo la Benki ya Posta Tawi
la Pamba wilayani Nyamagana huku chanzo cha mauaji hayo kikiwa hakijulikani.
Akizungumzia
tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Justus Kamugisha alisema kitendo
hicho si cha kawaida ndani ya jeshi hilo, na kufafanua jinsi mazingira ya tukio
lilivyotokea na kusababisha taharuki kwa wananchi na wateja waliokuwa ndani na
nje ya benki hiyo.
“Ni
kweli kuna askari wawili wamefariki eneo la Benki ya Posta. Katika eneo la
benki hiyo kulikuwa na askari wawili waliokuwa lindoni ambao ni PC Elisha na PC
Remigius Alphonce mwenye namba H 4291, wakiwa wanaendelea na lindo alifika
askari mwingine aliyekuwa amevaa kiraia PC Matiko na kuwasalimia kisha kuingia
ndani ya benki kuchukua fedha,”
alieleza Kamanda Kamugisha na kuongeza:
“Baada
ya dakika tano, Matiko alitoka nje na kuwaeleza askari wenzake kwamba mtandao
unasumbua, wakati akieleza hivyo, ghafla askari PC Elisha aliweka chemba risasi
ambapo mwenzake PC Alphonce alimhoji mbona unaweka risasi katika hali ya
utayari wa kutumika na alijibiwa kwa ufupi kwamba ‘achana na mimi.’
“Ghafla
alimfyatulia risasi PC Matiko na kumpiga eneo la bega la kushoto na kutokeza
mgongoni na kuanguka chini, kitendo hicho kilimfanya PC Alphonce kukimbilia
Benki ya Barclays ili kuomba msaada kwa askari wenzake waliokuwapo lindoni
hapo.
“Kabla
ya askari hao kufika, ilisikika sauti ya mlio wa risasi na baada ya kurudi
alimkuta PC Elisha akiwa amejipiga risasi kwenye paji la uso na kutokea nyuma
ya kisogo, tayari akiwa amepoteza maisha.”
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
.gif)


0 Responses to “ POLISI WAUANA KWA RISASI JIJINI MWANZA WAKIWA LINDONI”
Post a Comment