Wednesday, August 6, 2014
AUAWA KWA KUCHOMWA CHOMWA NA KITU CHENYE NCHA KALI MAKABURINI
Do you like this story?
Mtu mmoja ambaye
hajatambulika amekutwa ameuawa kwa kuchomwa chomwa sehemu mbalimbali za mwili
wake na kitu chenye incha kali katika makaburi ya misuna Singida mjini.
Wakielezea tukio hilo
balozi wa mtaa wa mwenge Bi. Mary Mwambusu na mwenyekiti wa mtaa wa misuna
Bwana Sarota Masawe wamesema tukio hilo linaonekana kutokea majira ya alfajiri
ya siku ya tarehe tano mwezi wa nane katika makaburi ya misuna.
Viongozi hao wa mtaa
Mwenge na Misuna wamesema tukio hilo ni la kwanza kutokea lakini wameliomba
jeshi la polisi kuimarisha ulinzi hasa maeneo kama hayo ilikudhibiti mauaji kama
hayo yasi tokee tena.
Akiongea kwa njia ya
simu kamanda wa jeshi la polisi mkoani Singida Bwana Geofrey Kamwela
amethibitisha kutokea kwa tukio hilo katika eneo la makaburi yaliyopo misuna
Singida mjini na amesema jeshi lake bado linaendelea na uchunguzi kuweza
kubaini chanzo cha mauaji hayo ambayo ni ya kinyama.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ AUAWA KWA KUCHOMWA CHOMWA NA KITU CHENYE NCHA KALI MAKABURINI”
Post a Comment