Sunday, December 6, 2015

SUMATRA YAENDESHA ZOEZI LA KUPIMA ULEVI KWA MADEREVA




Mamlaka ya udhibiti usafiri wa nchi kavu na majini ( SUMATRA ), imeendesha zoezi la ukaguzi la kupima ulevi kwa madereva wa mabasi ya abiria yaendayo mikoani na nchi jirani ya Uganda na kubaini kuwa kiwango cha ulevi miongoni mwa madereva hao kimeanza kupungua baada ya SUMATRA kwa kushirikiana na jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kwa madereva wasiozingatia sheria za usalama Barabarani.

Zoezi hilo la kupima ulevi kwa madereva limefanyika katika kituo kikuu cha mabasi cha Nyegezi jijini Mwanza kuanzia majira ya saa kumi na moja alfajiri,kabla ya mabasi kuanza safari za kuelekea mikoani na Kampala nchini Uganda, ambapo ITV imeshuhudia baadhi ya askari polisi wa kikosi cha usalama barabarani wakiendesha zoezi hilo.

Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya udhibiti usafiri wa nchikavu na majini ( SUMATRA ) Gilliard Ngewe amesema lengo la zoezi hilo ni kuwaelimisha abiria kutambua wajibu wao na haki zao wanapokuwa ndani ya vyombo vya usafiri, huku mmoja wa mawakala wanaokatisha tiketi za abiria katika stendi kuu ya mabasi nyegezi akiipa changamoto SUMATRA.

0 Responses to “SUMATRA YAENDESHA ZOEZI LA KUPIMA ULEVI KWA MADEREVA”

Post a Comment

More to Read