Sunday, December 6, 2015
WATUMISHI WA SERIKALI, SEKTA BINAFSI NA KAMPUNI MBALIMBALI JIJINI MBEYA WANATARAJIA KUADHIMISHA SIKU YA UHURU KWA KUFANYA USAFI
Do you like this story?
Kaimu mkurugenzi wa jiji la Mbeya Dr. Samwel Lazaro akiongea na waandishi wa Habari Ofisini kwake(Picha na David Nyembe wa Fahari News) |
Afisa wa idara ya usafirishaji na mazingira jiji, Samuel Bubegwa akielezea jinsi kuwa taasisi zitakazoshiriki kwenye zoezi la usafi(Picha na David Nyembe wa Fahari News) |
Waandishi wa Habari wakimskiliza Kaimu mkurugenzi wa jiji la Mbeya Dr. Samwel Lazaro(Picha na David Nyembe wa Fahari News) |
NA
SAMWEL NDONI MBEYA,
WATUMISHI
wa serikali,sekta binafsi na makampuni
mbalimbali jijini hapa wanatarajia
kuadhimisha siku ya uhuru kwa kufanya usafi kwenye maeneo waliyoelekezwa na
halmashauri ya jiji ikiwa ni utekelezaji
wa wa agizo la raisi Dr. John Magufuli.
Kaimu
mkurugenzi wa jiji la Mbeya Dr. Samwel Lazaro amesema kuwa kwa sasa jiji la
Mbeya linachangamoto ya kuwa na uchafu mwingi kutokana na mfumo wa ukusanyaji
taka unaotumika sasa
Amesema
halmashauri iliondoa maghuba na kuanzisha mfumo wa wananchi kukusanya taka
wanazozalisha kwenye maeneo yao na kutoa utaratibu kwa magari ya kuzoa taka
kupita kwenye maeneo hayo na kuziondoa taka hizo.
‘Changamoto
tunayoipata kwenye mfumo huu ni baadhi
ya watu wanakusanya takataka kwenye maeneo ya wazi kama vile barabarani hali
iliyopelekea maeneo mengi ya wazi kuwa machafu na hasa wakati huu wa mvua’’ amesema
Amesema
halmashauri ya jiji kwa sasa imeelezeza nguvu kwenye suala la usafi ambapo
tayari wamefanya usafi mkubwa kwenye soko la Soweto na kwamba utaratibu wa
kufanya usafi utakuwa mara moja kwa wiki.
Dr.
Lazaro amesema siku ya disemba 9, watumishi wa halmashauri wataadhimisha siku hiyo kwa kufanya usafi
kuanzia ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mbeya mpaka kwenye kituo kikubwa cha mabasi na
kuwataka madereva wote kuwa na vyombo maalum vya kuhifadhia taka.
Afisa
wa idara ya usafirishaji na mazingira jiji, Samuel Bubegwa amesema kuwa taasisi zitakazoshiriki kwenye zoezi la usafi
kwenye maeneo yao na maeneo mengine ni benki ya NBC, TTCL, kampuni ya simu ya
Airtel na vyuo vya Saut na TEKU pamoja na walimu wa shule ya sokondari Sangu.
Wengine
ni wafanyabiashara wadogo maarufu kama wamachinga, askari Magereza, polisi
wafanyakazi wa benki kuu, viongozi wa wilaya, wafanyabiashara wa masoko ya Sido
na Soweto pamoja na chama cha Mapinduzi CCM.
Aliongeza
kuwa wafanyakazi wa Hospitali ya rufaa Mbeya na hospitali ya wazazi meta
wameelekezwa kufanya usafi ndani ya Hospitali na maeneo yanayozunguka.
mwisho
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ WATUMISHI WA SERIKALI, SEKTA BINAFSI NA KAMPUNI MBALIMBALI JIJINI MBEYA WANATARAJIA KUADHIMISHA SIKU YA UHURU KWA KUFANYA USAFI”
Post a Comment