Friday, August 29, 2014
MGAWANYIKO WA MAPATO WATIKISA BUNGE MAALUMU
Do you like this story?
Dodoma.
Hoja kuhusu mgawanyo wa mapato ya muungano imeendelea kulitikisa Bunge Maalumu
la Katiba na jana watendaji wakuu wa wizara za fedha wa muungano na Zanzibar
pamoja na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Benno Ndulu walitua
Dodoma kuweka mambo sawa.
Vigogo
hao wa fedha jana walikutana na baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalumu, kujaribu
kupata mwafaka wa jinsi suala hilo litakavyowekwa kwenye Katiba Mpya.
Bunge
la Katiba limelazimika kuwaita Dodoma watendaji hao ili kusaidia kukwamua
mgogoro wa mapato ya muungano, ambao uliwagawa wajumbe wa kamati za Bunge hilo
wakati wa mjadala wa sura ya 14 kwenye Rasimu ya Katiba.
Pamoja
na Profesa Ndulu, wengine waliokuwapo ni Katibu Mkuu Hazina, Dk Servacius Likwelile
na mwenzake kutoka Zanzibar, Mussa Omar ambao walikuwa na kibarua kigumu cha
kupunguza ufa uliowatenga wajumbe wa Bunge hilo katika misingi ya Ubara na
Uzanzibari.
Sura
ya 14 ya rasimu ndiyo inayozungumzia masuala ya mapato ya muungano na mgawanyo
wake.
Suala
la mgawanyo wa mapato ni moja ya mambo manne magumu yaliyosababisha mvutano
mkubwa katika kamati za Bunge hilo kiasi cha kusababisha Kamati ya Uongozi ya
Bunge Maalumu kuunda kamati ndogo ili kulifanyia kazi.
Kutokana
na kusababisha mivutano hiyo, Kamati Namba Moja iliamua kutolijadili kabisa
suala hilo na badala yake, kuomba uongozi wa Bunge uwalete watendaji wakuu wa
masuala ya fedha ili watoe mwongozo wa kuwawezesha wajumbe kujadili na kupata
mwafaka wa jinsi fedha zitakavyoweza kusimamiwa na kugawanywa. Mwenyekiti wa
kamati hiyo ambaye pia ni Naibu Waziri - Ofisi ya Makamu wa Rais, Ummy Mwalimu
alisema walishindwa kupigia kura sura ya 14 baada ya kuona ina utata.
“Ni
kweli hatukupigia kura sura ya 14 pekee, tuliona ina utata mkubwa ambao unahitaji
ufafanuzi wa kina na bila shaka baada ya semina ya leo (jana) tutakutana
kufanya uamuzi,” alisema Mwalimu.
Katibu
wa Bunge Maalumu, Yahya Hamis Hamad alisema: “Kamati zote zimemaliza kazi,
isipokuwa Namba Moja haikupigia kura sura ya 14 wakitaka ufafanuzi wa
kitaalamu, ndiyo maana tumewaleta wataalamu leo.”
Alisema
pamoja na kupigia kura sura hiyo, lakini hata kamati nyingine zilionekana
kutoelewa vizuri sura hiyo, hivyo ujio wa wataalamu ulilenga kuwawezesha
kujadili sehemu hiyo ya Katiba wakiwa na uelewa mpana.
Habari
zinasema sura iliyojitokeza kwenye mijadala ya kamati zote 12 ilihamia kwenye
semina hiyo, ambako ufa ulidhihirika baina ya wajumbe wa pande hizo mbili za
muungano, lakini watendaji hao kwa kushirikiana na wataalamu wengine
walifanikiwa kutoa mwelekeo wenye matumaini.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MGAWANYIKO WA MAPATO WATIKISA BUNGE MAALUMU”
Post a Comment