Thursday, August 21, 2014
MWENYEKITI WA BUNGE MAALUM LA KATIBA AUNDA KAMATI NDOGO.
Do you like this story?
Na Magreth Kinabo, Dodoma
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta ameunda kamati ndogo
yenye ujumbe wa watu 10 kwa ajili ya kushughulikia masuala ambayo
hayakufikia muafaka wakati wa majadiliano ya kupitia sura mbalimbali za
Rasimu ya Katiba Mpya kwenye Kamati 12 za Bunge hilo.
Kamati hiyo itakuwa inaongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Bunge hilo, Mhe.
Samia Suluhu Hassan,ambapo wajumbe wa kamati hiyo wametoka kila
pande ya Muungano yaani watano wametoka Tanzania Bara na watano kutoka
Zanzibar.
Aidha Mhe. Sitta akizungumzia kuhusu maendeleo ya kazi za
Kamati hizo, ambapo alisema zinaendele vizuri, hivyo kuanzia wiki ijayo
sura zote 15 zitakuwa zimepigiwa kura,hivyo Kamati hizo zitakuwa
zimemaliza sura 17 ya rasimu hiyo na za nyongeza ifikapo Agosti 27,mwaka huu
ili kuanza kuwasilisha katika Bunge hilo kuanzia Septemba 2,mwaka huu.
Hayo yalisemwa leo na Mhe. Samuel Sitta wakati akizungumza na
waandishi wa habari alipokutana nao Kuongea kuhusu muhtasari wa kikao cha Kamati ya
Uongozi wa Bunge hilo kilichokaa kutathmini kazi za Kamati 12 za Bunge hilo
lilipofikia pamoja kuridhia baadhi ya mapendekezo ya kuongeza Ibara na sura
ndani Rasimu ya Katiba katika Kamati zao.
Mwenyekiti huyo aliyataja mambo ambayo yatashughulikiwa na kamati hiyo,
ni muundo wa Bunge katika masuala ya Muungano, uraia pacha,
mahakama ya kadhi na kamati ya pamoja ya fedha.
“Haya mambo manne nimeagiza ufanyike utaratibu maalum,” alisema Mhe.
Sitta.
Mhe . Sitta akizungumzia kuhusu tathimini ya mwenendo wa
Kamati hizo, alisema zipendekeza masuala kadhaa na kuacha mengine kama
yalivyo katika rasimu hiyo.
Akizungumzia kuhusu yaliyojadiliwa katika kikao cha Kamati ya Uongozi ya
Bunge hilo,kabla ya kukutana na waandishi wa habari, Mhe. Sitta alisema kamati
hiyo imepokea mapendekezo kutoka katika kamati mbalimbali kuhusu kuongezeka kwa
sura na Ibara za rasimu hiyo.
Aliyataja mapendekezo hayo , likiwemo la Tume ya Marekebisho ya
Katiba lililowasilisha na Jaji Warioba kuhusu ardhi, mazingira na rasilimali za
taifa, Jumuia ya Tawala za Serikali za Mitaa (ALAT) na pendekezo la
Haki ya Watumiaji huduma na bidhaa ili kuwalinda walaji lililowasilishwa , Hawa
Ng’umbi ambaye ni mjumbe wa Bunge hilo.
Aliyataja mapendekezo mengine ni la Jukumu la
Serikali kujenga uchumi imara, ambapo lengo ni kuwa na maendeleo ya uchumi wa
ujamaa na kujitegemea na Kuwepo kwa Baraza la Habari, la wajumbe wa 201 kuhusu
ardhi, wafugaji, wavuvi pia na wachimbaji wadogo ili ziweze kutungwa Sheria za
kusimamia masuala hayo.
Mhe. Sitta alisema kutokana na mapendekezo hayo kutakuwepo na
ongezeko la ukurasa na sura kadhaa katika rasimu hiyo.
Alisema Kamati imebaini tatizo la mahudhurio, aliwapongeza wajumbe
wa Bunge hilo kutoka upande wa Zanzibar kwa kuwa na mahudhurio mazuri kwenye
vikao kuliko kutoka Tanzania Bara kuacha visingizio vya kutohudhuria
vikao.
Katika hatua nyingine Mhe. Sitta alisema kutakuwepo na wataalamu
kabla ua kumalizika kwa wiki hii kwa ajili ya kutoa ufafanuzi wa
mambo kadhaa kutoka Hazina kwa pande zote za Muungano, ambapo ataukuwepo
pia Gavana wa Benki Kuu, Profesa Bonaventure Rutinwa kwa ajili ya suala la
uraia pacha, uhamiaji na Profesa Issa Shivji ambaye ataoa ufafanuzi juu
ya aina ya Muungano ili kuwa na uwiano kwa kuwa hivi sasa yapo mambo machache.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MWENYEKITI WA BUNGE MAALUM LA KATIBA AUNDA KAMATI NDOGO.”
Post a Comment