Tuesday, August 19, 2014
UAMUZI MGUMU CCM KATIKA KAMATI KUU LEO
Do you like this story?
Dodoma/Dar. Kamati Kuu (CC) ya Halmashauri Kuu ya CCM inakutana
leo mchana mjini Dodoma chini ya mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete huku
ikitarajiwa kufanya uamuzi mgumu wa mchakato wa Katiba.
Kikao
hicho kinaketi mara ya pili katika muda mfupi, baada ya hivi karibuni kukaa
jijini Dar es Salaam na kueleza kuridhishwa na mchakato huo.
Hata
hivyo, safari hii kikao hicho kinaketi kukiwa na maswali lukuki ambayo
hayajapata majibu: Je, Bunge la Katiba liendelee au livunjwe? Je, lisitishwe
kwa muda kupisha maridhiano au la? Je, kuna umuhimu wa maridhiano? Kuna ulazima
wa kuwapo Ukawa bungeni?
Akizungumzia
kikao hicho, mtaalamu wa sayansi ya siasa na utawala katika Chuo Kikuu cha Dar
es Salaam, Dk Alexander Makulilo alisema jambo kubwa litakalojadiliwa katika
kikao hicho ni kauli tofauti zilizotolewa na wananchi kuhusu mchakato wa kupata
Katiba Mpya.
“Naibu
Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba ameshauri yafanyike maridhiano kwanza na
wapo wanaCCM waliomuunga mkono. Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Frederick
Werema naye ameonyesha wasiwasi wake, Ukawa na Jukwaa la Katiba Tanzania nao
wamesema yao. Nadhani kuna jambo CCM wameliona na wanataka kuliweka sawa,”
alisema Dk Makulilo.
Aliongeza,
“Kujua nini wataamua ni ngumu lakini kutokana na hali ilivyo kwa sasa ni wazi
kuwa wanakutana kuona nini kifanyike.”
Kwa
upande wake Bashiru Ali alisema, “Tangu mwanzo mchakato wa Katiba haukuwa
katika ilani ya CCM, sasa unaweza kujiuliza wanakwenda kujadili nini wakati
hata katika mikakati yao ya miaka 10 na 20 ijayo hakuna mpango wa kuandika
Katiba.”
Habari
zilizozagaa mjini Dodoma zinadai kikao hicho pia kinaweza kupendekeza
kuwashughulikia wanachama wake waliotoa kauli zinazopingana na msimamo wa chama
hicho.
Miongoni
mwa waliotoa kauli zinazopingana na chama hicho ni Naibu Katibu Mkuu Tanzania
Bara, Mwigulu Nchemba kutokana na matamshi yake ya kuhoji uhalali wa vikao vya
Bunge la Katiba kuendelea bila uhakika wa akidi.
Mbali
na Mwigulu pia wabunge kadhaa wa CCM akiwamo, Esther Bulaya (Viti Maalumu),
Kangi Lugora (Mwibara), Deo Filikunjombe (Ludewa), Ridhiwani Kikwete (Chalinze)
nao wamekaririwa kwa nyakati tofauti wakitoa misimamo inayokinzana na chama
chao kuhusu uhalali wa Bunge la Katiba kuendelea bila kuwapo maridhiano na
Ukawa.
Hata
hivyo, habari nyingine zinasema iwapo kuna mpango huo, Mwigulu anaweza
kuondolewa kutokana na utaratibu wa chama hicho kuwaondoa kwenye sekretarieti
wajumbe wake wanaoteuliwa kushika nyadhifa serikalini.
Chanzo
chetu kinasema ikiwa hilo litatokea kwa sababu ya Mwigulu kuteuliwa Naibu
Waziri wa Fedha, basi mpango huo hautamwacha nyuma Katibu wa Siasa na Mambo ya
Nje, Dk AshaRose Migiro ambaye pia hivi karibuni aliteuliwa kuwa Waziri wa
Sheria na Katiba.
Via
>Mwananchi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “UAMUZI MGUMU CCM KATIKA KAMATI KUU LEO”
Post a Comment