Wednesday, August 13, 2014
WANAWAKE WAYAZUIA MAGARI YA JESHI KUPINGA WAUME ZAO KUPELEKWA KUPAMBANA NA BOKO HARAM.
Do you like this story?
Ripoti
kutoka Nigeria zinaeleza kuwa Jumamosi iliyopita kundi kubwa la wanawake
lilijitokeza na kuzuia magari ya jeshi yaliyokuwa yamewabeba wanaume wao na
wake zao yakielekea katika mji wa Gwosa, sehemu ambayo inadhibitiwa na kundi la
Boko Haram.
Kwa mujibu
wa Prime Times ya Nigeria, wanawake hao walizua geti la barracks katika mji wa
Borno huku wengine wakilala barabarani kushinikiza waume zao wapewe vifaa vya
kisasa na imara zaidi ndipo waende vitani kupambana na kundi hilo.
Hali hiyo
imekuja baada ya kuripotiwa kuwa karibu wanajeshi 60 waliuawa Jumatano
iliyopita katika eneo la Gwosa linalomilikiwa na Boko Haram na kudaiwa kuwa
sababu kubwa ni zana duni walizokuwa nazo kulinganisha na zana za kisasa za
kijeshi za kundi hilo.
Chanzo
kimeiambia Prime Times kuwa wanawake hao walieleza kuwa hawataki kubaki wajane
na yatima kama wenzao kwa sababu ya vita hiyo.
“Mwanamke
mmoja alisema ‘hatutaki kuwa kundi lingine la wajane, wapeni waume zetu zana
bora zaidi za kivita, silaha na magari bora zaidi la sivyo hawaendi kokote’.”
Wanajeshi
wengine pia walionekana kuunga mkono madai ya wanawake hao na kusukuma lawama
kwa maafisa wa serikali.
Kundi la
Boko Haram bado linawashikilia mateka wanafunzi wa kike zaidi ya 200 na
wanawake wengine huku likitekeleza mauaji ya kutisha katika maeneo mbalimbali
ya nchi hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WANAWAKE WAYAZUIA MAGARI YA JESHI KUPINGA WAUME ZAO KUPELEKWA KUPAMBANA NA BOKO HARAM.”
Post a Comment