Wednesday, August 13, 2014
KIKAO CHA MKAKATI WA UJENZI WA MAABARA ZA SHULE ZA SEKONDARI ZA KUDUMU KATA CHAFANYIKA DAR ES SALAAM
Do you like this story?
Mchumi, wa Manispaa ya Kinondoni, Bw.Salm Hamisi Msuya akielezea mchakato wa uchangiaji wa ujenzi wa maabara katika shule 18 za sekondari zilizokuwa na maabara za kudumu wakati wa kikao hicho. |
MANISPAA ya Kinondoni
inahitaji jumla ya kiasi cha Sh Bilioni 1.3 ili kutekeleza agizo la Rais Jakaya
Kikwete aliyezitaka Halmashauri zote kuhakikisha zinajenga maabara katika
shule za Sekondari ifikapo Novemba Mwaka huu.
Hayo yamebainishwa jana Jijini
Dar es salaam na Naibu Meya wa Manispaa hiyo Songoro Mnyonge wakati
akizungumza katika kikao kilichowakutanisha wadau mbalimbali wakiwemo wakuu wa
shule, watendaji wa mitaa, kata pamoja na wenyeviti wa bodi za shule chenye
lengo la kuangali namna ya kupatikana kwa fedha hizo.
Huku akiwaomba wadau mbalimbali
yakiwemo mashirika, taasisi, watu binafsi pamoja na wafanyabiashara kujitokeza
kuchangia upatikanaji wa fedha hizo, Songoro alisema ushirikiano wao katika
suala hilo utaipa faraja manispaa hiyo kutokana na umuhimu wa elimu kwa
taifa.
“Tunawaomba mjitokeze kwa wingi
ili kuunga mkono juhudi za Rais Kikwete anayetaka kuona shule zote za sekondari
zinakuwa na maabara za kudumu ili kusaidia kupanua wigo wa ufundishaji kw
wanafunzi mashuleni, jitihada zetu pekee hazitotuwezesha kufikia malengo hayo
kutokana na ufinyu wa bajeti” alisema Mnyonge.
Aidha alisema manispaa hiyo
inahitaji maabara za kudumu 114 kukidhi mahitaji katika kata 32 huku sekondari
14 ndizo pekee katika zilizo na maabara hizo kati ya 46 zilizopo katika
manispaa hiyo suala alilosema linahitaji kutafutiwa ufumbuzi wa haraka.
Alisema kila chumba kimoja cha
maabara ya kudumu ujenzi wake unakadiriwa kufikia kiasi cha Sh Milioni 75 na
kwa jumla ya vyumba vote 114 inahitajika kiasi hicho cha zaidi ya Sh Billioni
1,suala alilosema haliwezi kufanikiwa bila nguvu za wadau mbalimbali.
Alisema malengo ya baadae ya
manispaa hiyo ni kujenga vyumba vitatu vya maabara ya fikizia, kemia na
baiolojia ifikapo mwaka 2016 hatu aliyosema kwa kiasi kikubwa itamaliza tatizo
la ugumu wa masomo ya sayansi kwa wanafunzi sambamba na kuongeza wataalam wa
baadae wa Taifa hili.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “KIKAO CHA MKAKATI WA UJENZI WA MAABARA ZA SHULE ZA SEKONDARI ZA KUDUMU KATA CHAFANYIKA DAR ES SALAAM”
Post a Comment