Thursday, September 25, 2014
MIZUKA YA FIESTA MBEYA IMEWADIA............... MPANGO MZIMA HUU HAPA;
Do you like this story?
![]() |
|
Mtangazaji wa kipindi cha Jahazi
Mussa Husein akitoa ratiba nzima ya Serengeti Fiesta katika mahojiano
yake ndani ya Generation Fm Mbeya.
|
![]() |
| Mtangazaji wa Generation Fm Twal B akiwa na Feeby wakiongea na mratibu wa Serengeti Fiesta Bw Mussa Husein |
Kwa mwaka 2014 hakika wakazi wa
jiji la mbeya na vitongoji vyake utakuwa ni mwaka wa kihistoria kwao
kutokana na kufunguliwa tena kwa pazia la burudani yanii Serengeti
Fiesta 2014 nisheedah ikihusisha burudani mbalimbali kama Serengeti Soka
Bonanza pamoja na Serengeti Diva Supar Nyota bila kuwasahau wazee wa fursa.
Mmoja wa waraatibu wa shughuli
nzima ya Serengeti Fiesta 2014 kwa Mkoa wa Mbeya Bw.Mussa Hussein amesema
tayari kwa kiwango kikubwa maandalizi ya burudani hizo zimefikia katika hatua
nzuri ambapo kwa sasa burudani hizo zimeanza na hatua ya utoaji wa zawadi kwa
wadau ambao wamekuwa wakishiriki moja kwa moja katika mchakato huo wa
serengetoi fiesta 2014 jijini hapa.
Akitoa ratiba nzima ya Sherehe
hizo Mussa amesema septemba 26 mwaka huu kutakuwa na Bonanza litakalo husisha
Timu 4 kutoka katika bar mbalimbali za jiji la Mbeya ambapo mshindi wa
kwanza katika bonanza hilo atapatiwa zawadi ya Katoni kumi za Bia kutoka
Serengeti huku mshindi wa pili akipatiwa katoni 5 bonanza ambalo litafanyika
katika viwanja vya chuo cha uhasibu T.I.A .
Amesema bonanza hilo lifanyika
kwa lengo la kuamsha hisia za wakazi wa jiji la mbeya katika kuelekea kilele
cha Serengeti Fiesta 2014 katika viwanja vya Sokoine siku ya jumapili Septemba
28 mwaka huu.
Aidha Mratibu huyo amesema mara
baada ya kukamilika kwa Fiesta Soka Bonanza kutakuwa Serengeti Pree Party
itakayo fanyika katika ukumbi wa Babiz Cafee ambayo itahudhiriwa ana wasanii
mbalimbali watakao pata fursa ya kupafom katika show ya Serengeti Fiesta
Sokoine kwa kiingilio cha shilingi 5000.
Amesema Septemba 28 mwaka huu majira
ya saa 4 asabuhi kutakuwa na Serengeti Diva supar Nyota ndani ya ukumbi huo wa
Babiz ambapo baadaye majira ya saa 8 mchana kutakuwa na semina za fursa katika
ukumbi wa mikutano wa Mkapa semina ambazo zitaongozwa na Bw.Luge pamoja na
wadau mbalimbali.
Hata hivyo Bw.Mussa ametoa wito
kwa wakazi wa jiji hilo kujitokeza kwa wingi katika kilele cha burudani hizo
huku akiwataka wakazi hao kuondoa hofu juu ya kuwepo kwa uharibifu wa uwanja wa
sokonie kwani burudani nzima hazita husika katika eneo la pichi la uwanja huo
hasa kutokana na kuwepo kwa ulinzi mkali pamona eneo zima kuzungushiwa kamba
ili kuzuia kabisa uhalibifu wa uwanja huo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
.gif)




0 Responses to “MIZUKA YA FIESTA MBEYA IMEWADIA............... MPANGO MZIMA HUU HAPA;”
Post a Comment