Wednesday, September 3, 2014
UNYAMA MKUBWA: MUME WA WAKE WAWILI ASIMULIA ALIVYOLAWITIWA KINGUVU NA WANAUME 6 GESTI
Do you like this story?
![]() |
Mmoja wa watuhumiwa wanaoshikiliwa na polisi kuhusiana na kesi hiyo. |
Hatimaye yule
mwanaume aliyedaiwa kufumaniwa na mke wa mtu na hatimaye kufanyiwa usodoma
na watu sita, akiwemo mume wa mwanamke huyo amefungukia mchezo mzima.
Hivi karibuni
mwanaume huyo (jina tunalo) ambaye ni mume wa wake wawili na mkazi wa Yombo
Kiwalani, Wilaya ya Ilala jijini Dar mwenye umri wa miaka 34 alikutwa na
mkasa huo kwenye nyumba ya kulala wageni iitwayo Yombo Executive inayomilikiwa
na Athuman Maembe.
Mara baada ya picha
za tukio hilo kuenea kwenye mitandao ya kijamii na watu kushangaa, gazeti hili
lilituma timu yake ya habari za uchunguzi ili kupata ukweli wa tukio hilo.Uwazi
lilifanikiwa kumpata mwanamume huyo ambaye ni mfanyabiashara, pia
alijitambulisha kuwa yeye ni mwelimishaji rika wa magonjwa ya ngono, afya ya
uzazi, madawa ya kulevya na unyanyasaji wa kijinsia.
Alianza kwa kusema:
“Ni kweli mimi ndiye niliyetendewa ukatili ule. Natamani kujiua kwani mambo
yale nayasikia tu usiombe yakukute.
“Nimefedheheka sana,
sina mahala pa kuficha aibu hii kubwa. Kila nikikumbuka kuwa nina wake wawili
na watoto, wazazi, marafiki na ndugu, bora hata wangeniua kuliko kuniacha
nazidi kudhalilika hivi.
“Siku ya tukio ilikuwa Jumamosi ya Agosti 23, mwaka huu. Kuna mwanamke mmoja anaitwa mama Lilly alinipigia simu. Kwanza alikuwa akinipigia simu mara kwa mara wiki moja kabla ya tukio akinieleza kwamba ana shida na mimi, alisema mume wake amekuwa akimnyanyasa kijinsia.
“Siku hiyo, saa tatu
asubuhi mama Lilly alinipigia simu huku analia, akasema kwamba mumewe
kampiga na kumfukuza nyumbani hivyo anaomba kuonana na mimi kwa ajili ya
ushauri ila alitaka tukutane naye maeneo ya Mtongani, Mbagala au Tandika.
“Nilikataa,
nikamwambia aje kwenye Ukumbi wa Maembe ninakotoaga mafunzo mbalimbali kwa
vijana. Ukumbi huo upo karibu na nyumba hiyo ya kulala wageni kulikotokea
tukio.
“Huyu mwanamke namfahamu kwani kipindi cha nyuma alikuwa na stationary karibu na maeneo haya, nilikuwa nikimtengenezea kompyuta lakini miaka miwili iliyopita alihama na sikujua alipo hadi hivi karibuni aliponipigia simu.
“Basi, nilipomwambia
aje yeye maeneo haya, aliamua kunifuata. Alifika saa saba mchana huku
akibubujikwa machozi, nilimsikiliza kwa makini matatizo yake mwishowe aliniomba
nimkopeshe shilingi laki moja ili aende kwao, nilimjibu kwa pale sikuwa nazo
labda mpaka Jumatatu.
“Akasema kama ni
hivyo basi nimsaidie sehemu ya kulala ili kesho yake aondoke kwenda kwa dada
yake. Nilimuonea huruma, nilimchukulia chumba, nikamwambia kama kutakuwa na
tatizo anipigie simu. Wakati najiandaa kutoka chumbani aliendelea kuongea
maneno mengi sana ya kunifanya niendelee kuwepo.
“Wakati huo alikuwa
akituma ujumbe wa simu sehemu nisiyoijua. Sasa nilipoagana naye, ile natoka tu,
mlangoni niliona wanaume sita wakanirudisha chumbani na kufunga
mlango.“Wakaniambia niwape namba yangu ya akaunti ya benki na password ya simu
yangu kwani walijua kwamba tayari nimetumiwa fedha kutoka nje ya nchi kutoka
kwa wafadhili.
“Niliwaambia sina
akaunti, wakanipiga sana, ikabidi niwaongopee kwamba nyumbani nina shilingi
laki tano, wakaniambia niwaelekeze nyumbani, nikafanya hivyo. Wawili kati yao
waliondoka na pikipiki hadi kwangu kuchukua fedha, wengine wakawa wamenizuia
chumbani na kunitishia nikipiga kelele ndiyo mwisho wa maisha yangu.
“Wale walipofika
kwangu walimwambia mke wangu awape laki tano na walimtaka aongee na mimi kwa
simu huku nikiwa chini ya ulinzi. Mke wangu aliwaambia hana fedha hizo ana laki
moja tu, nilimwambia awape.“Waliporudi na shilingi laki moja walisema
nimewadanganya, wakaniadhibu na kunivua nguo, wakanilawiti kwa zamu na
kunilazimisha kuwafanyia mambo ambayo ni tabu hata kuyasema huku wakinipiga
picha.
“Baada ya kumaliza
walichukuwa laptop, nguo na simu wakaondoka huku wakiniambia ifikika Jumatatu,
yaani siku moja baada ya tukio niwape shilingi milioni moja la sivyo wanaweka
picha zangu mtandaoni.
“Hata hivyo, baada ya
kukosa hizo fedha waliziweka picha mtandaoni, ikawa napigiwa simu na watu
mbalimbali walioziona.“Waliponiacha pale chumbani nikiwa sina nguvu,
nilichukuwa shuka nilijikokota mpaka kwa meneja wa gesti na kumweleza. Alinipa
nguo yake ili niweze kwenda Kituo Kidogo cha Polisi cha Minazi Mirefu kutoa
taarifa na baadaye Buguruni na kufungua kesi yenye jalada namba BUG/RB/8520/2014
Kujipatia Fedha kwa Njia ya Udanganyifu lakini baadaye ikaongezwa shitaka
lingine la kulawiti.
“Kinachonishangaza ni
kwamba iweje wanaume hao sita waingie na kutoka bila wenye gesti kuwabaini?”
alihoji mwanaume huyo.
Naye mmiliki wa
nyumba hiyo ya wageni alikiri kupokea taarifa ya kutokea kwa tukio hilo na
kudai kwamba ni la aibu na kusema suala hilo linashughulikiwa na jeshi la
polisi.
Kamanda wa Mkoa wa
Kipolisi Ilala, SACP, Mary Nzuki alipohojiwa na mmoja wa waandishi wa habari
hii ofisini kwake mwishoni mwa wiki iliyopita alikiri kutokea kwa tukio hilo na
kusema tayari watuhumiwa wanne wanashikiliwa Kamanda Nzuki aliwataja
wanaoshikiliwa kuwa ni Erick Kasila, Sanifa Sadik, Shela Sadik na Juma Richard.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ UNYAMA MKUBWA: MUME WA WAKE WAWILI ASIMULIA ALIVYOLAWITIWA KINGUVU NA WANAUME 6 GESTI”
Post a Comment