Thursday, August 27, 2015
POLISI KUTOA TAMKO KUHUSU MUDA WA KAMPENI.
Do you like this story?
Jeshi la Polisi
nchini Tanzania limesema kuwa litatoa tamko la jeshi hilo juu ya Chama cha
Mapinduzi kuzidisha muda wakati wa Uzinduzi wa Kampeni za chama hicho wiki
iliyopita.
Akizungumza na
waandishi wa habari wakati wa mdahalo wa wadau wa uchaguzi jana jijini Dar es
salaam Kamishna wa Mafunzo na Operasheni wa Jeshi la Polisi CP Paul Chagonja
amesema kuwa wanashughulikia suala hilo na muda ukifika watatoa tamko.
Ameongeza kuwa ili
uchaguzi uwe wa Amani ni lazima watu wote watimize wajibu wao.
Kwa upande wa Tume ya
Taifa ya Uchaguzi iliwakilishwa na Jaji Mstaafu John Mkwawa alivitaka vyama vya
siasa kuzingatia maadili ya uchaguzi waliosaini ili kulinda amani na kuepusha
migogoro na uvunjifu wa Amani.
Kwa upande wa
mwakilishi toka chama cha ADC Mwanaisha Yemba alivitaka vyama vyenye vikundi
vya ulinzi kuwapa sare na alama maalum walinzi wao ili watambuliwe na kila mtu
ili wakifanya vujo iwe rahisi kutambulika.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ POLISI KUTOA TAMKO KUHUSU MUDA WA KAMPENI.”
Post a Comment