Tuesday, November 4, 2014
MWAKIBINGA AONDOKA BODI YA LIGI
Do you like this story?
Na Boniface Wambura, Dar es salaam
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Silas
Mwakibinga amemaliza mkataba wake tangu Oktoba 31 mwaka huu.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na TPLB wanamshukuru
Mwakibinga kwa mchango wake kwa kipindi ambacho ameitumikia Bodi, na kumtakia
kila la kheri katika majukumu yake mapya huko aendako.
TPLB hivi sasa iko katika mchakato wa kupata Ofisa Mtendaji Mkuu
mpya kwa ajili ya kuziba nafasi hiyo iliyoachwa wazi na Mwakibinga baada ya
muda wa mkataba wake kumalizika
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MWAKIBINGA AONDOKA BODI YA LIGI”
Post a Comment