Thursday, March 9, 2017

WATOTO 19 WAFARIKI KATIKA KITUO CHA MALEZI


 
Moto uliotokea katika kituo cha kulelea watoto kinachosimamiwa na serikali, Guatemala umewaua takribani watoto kumi na tisa huku wengine 25 wamejeruhiwa.Watoto takriban 60 wametoroka wakisema kuwa wamekuwa wakinyanyasika.
Bado haijafahamika ni nini chanzo cha moto huo lakini taarifa za awali zinaonyesha kuna uwezekano moto huo umewashwa kwa makusudi na wakazi wa nyumba hiyo, kama anavyoeleza afisa wa kikosi cha kuzima moto Jorge Mario Cruz
''wakazi kadahaa wamesababisha moto huu katika maeneo mawili, hivyo kikosi cha kuzima moto wakatumwa kupambana na moto huo na kusaidia kutoa huduma ya kwanza,tumefanikiwa kuuzima kwa kutumia magaloni ya maji zaidi ya 3000, kuna wakazi takriban 25 waliojeruhiwa''
  Ndugu na jamaa wa watoto wa walioathirika na moto ,wamekusanyika nje ya kituo cha Guatemala
Wabunge wa nchi hiyo wametaka uchunguzi wa haraka kufanyika kuhusu tukio hilo katika kituo cha Guatemala .Huku rais wa Guatemala,Jimmy Morales ametoa siku tatu za maombolezo.
Siku za nyuma,makazi hayo yamewahi kupata lawama za kuwa kituo cha manyanyaso. Makazi hayo yamekuwa yakitunza watoto wapatao takribani mia tano ambao wamekuwa waathirika wa vurugu (ingawa eneo hilo lilitengenezwa kuwatunza watoto mia nne pekee)

0 Responses to “WATOTO 19 WAFARIKI KATIKA KITUO CHA MALEZI”

Post a Comment

More to Read