Thursday, March 9, 2017

BABA AFUNGA KITOVU CHA MTOTO WAKE NA KAMBA YA KIATU


Mtoto Saphia alikuwa amepitisha tarehe yake ya kuzaliwa kwa wiki mbili
Ilimlazimu baba kutumia kamba ya kiatu kufunga kitovu cha mtoto wake baada ya mkewe kujifungua akiwa ndani ya gari lao.
Paul Doherty na mkewe Georgina, walikuwa njiani kuenda hospitalini wakati walilazimika kusimamisha gari kando ya barabara.
Aliwapigia simu watoa huduma za dharura ambao walizungumza naye huku mkewe akijifungua.
"Ghafla mtoto akatoka, kwa hivyo ilinilazimu kuweka simu chini ili nimshike."
"Nikampa Georgina mtoto na akaanza kulia. Kisha wakaaza kunishauri nihakikishe kuwa wote wamepata joto, ni nifunge kitovu."
"Ilinilazimu kuchukua kamba ya kiatu changu, kwa sababu ndiyo tu nilikuwa nayo kwenye gari," Doherty alisema.
"Ilianza siku ya Jumamosi asubuhi wakati nilianza kuhisi uchungu mwendo wa saa 11:30 kisha nikajifungua 14:40, kwa hivyo ilikuwa ni kitu cha haraka. alisema Georgina.
Tulikuwa tumepita Bridgend wakati nilimuomba mume wangu kusimamisha gari kando, nilijua kuwa singefika hospitalini.

0 Responses to “BABA AFUNGA KITOVU CHA MTOTO WAKE NA KAMBA YA KIATU”

Post a Comment

More to Read