Thursday, March 9, 2017
BARCELONA YAANDIKA HISTORIA
Do you like this story?
Barcelona wamebirua matokeo ya kutinga nusu fainali kwa kuizaba Paris Saint Germain kwa mabao 6-1 katika mchezo wa marudiano wa Klabu Bingwa Ulaya.
Sergi Roberto alifunga bao la 6 kwa mkwaju wa mwisho
wa mchezo, na hivyo kufanya matokeo ya jumla kuwa 6-5 kwenye mchezo
uliopigwa kwenye dimba la Nou Camp.
Barcelona walifunga magoli matatu katika dakika saba za mwisho. Walikuwa wakiongoza kwa 3-1.
Wiki tatu zilizopita PSG iliifunga Barcelona magoli 4-0 mjini Paris.
Hatua
ya kurejesha magoli yote hayo ni kubwa kuwahi kushuhudiwa katika
historia ya UEFA, na sasa Barcelona wana kila nafasi ya kunyanyua kombe
la Klabu Bingwa Ulaya kwa mara ya pili katika kipindi cha miaka mitatu.
Katika
mchezo mwingine, Pierre Emerick Aubameyang alipachika 'hat trick' na
kuipeleka Borussia Dortmund katika robo fainali dhidi ya Benfica.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “BARCELONA YAANDIKA HISTORIA”
Post a Comment