Thursday, September 29, 2016
TRUMP APOTEZA $800m KIPINDI CHA MWAKA MMOJA
Do you like this story?
Mfanyabiashara
tajiri wa New York anayewania urais kupitia chama cha Republican nchini
Marekani Donald Trump amepoteza $800m ya utajiri wake katika kipindi cha mwaka
mmoja, kwa mujibu wa jarida la Forbes.
Jarida
hilo linasema kwa sasa utajiri wa Bw Trump ni $3.7bn (£2.7bn).
Forbes
wanasema kushuka huko kwa thamani ya utajiri wake kunatokana na 'kudorora kiasi'
kwa biashara ya nyumba na ardhi katika soko la New York.
Bw
Trump, ambaye wakati mmoja liandika kitabu kwa jina Midas Touch (Mguso wa
Midas: Midas aliaminika kubadilisha kila alichogusa kuwa dhahabu), amekuwa
akisema kwamba rais wa Marekani kwa sasa anaweza kuwa mtu mwenye busara katika
biashara na majadiliano.
Wakati
wa mdahalo wa urais Jumatatu, alisema: "Nina mapato makubwa ... wakati
umefika kwa taifa hili kuwa na mtu anayefahamu mengi kuhusu pesa."
Forbes,
ambao wamekuwa wakikadiria utajiri wa Bw Trumo kwa zaidi ya miongo mitatu,
wanasema hilo limetokana na kudorora kwa soko la nyumba, afisi na ardhi New
York.
Kati
ya majumba 28 ambayo yalichunguzwa na Forbes, 18 yalishuka thamani, likiwemo
jumba maarufu la Trump Tower linalopatikana Manhattan.
Jumba
lake lililo 40 Wall Street na kilabu chake cha Mar-a-Lago kilichopo Palm Beach,
Florida, pia vilipoteza thamani, kwa mujibu wa Forbes.
Lakini
majumba saba ya Trump, likiwemo jumba la pili kwa urefu San Francisco, yalipanda
thamani.
Inakadiriwa kwamba amewekeza $50m, pesa zake binafsi, kwenye
kampeni kufikia sasa.
Forbes wanakadiria kwamba matamshi yake dhidi ya wahamiaji wa
Mexico yalimgharimu $100m kupitia mikataba aliyopoteza kwenye mashirika makubwa
kama vile NBC Universal, Univision na Macy's.
Utajiri
wake kamili haujulikani. Alipowasilisha taarifa zake za kifedha kwa Tume ya
Dola ya Uchaguzi, alisema ana "zaidi ya dola bilioni kumi."
Lakini
Forbes wanasema utajiri wake ni $3.7bn, Bloomberg wanasema anamiliki $3bn nao
Fortune wanasema ana $3.9bn.
Moja
ya sababu inayochangia hili ni kwamba Bw Trump pia huhesabu thamani ya jina
lake, ambalo anakadiria kwamba thamani yake ni karibu $3.3bn.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ TRUMP APOTEZA $800m KIPINDI CHA MWAKA MMOJA”
Post a Comment