Thursday, September 29, 2016
BEI YA MAFUTA DUNIANI YAANZA KUPANDA BAADA YA MAAFIKIANO OPEC
Do you like this story?
Bei ya mafuta duniani imeanza
kupanda baada ya muungano wa mataifa yanayozalisha mafuta kwa wingi, Opec,
kukubaliana kupunguza uzalishaji wa mafuta kwa mara ya kwanza katika kipindi
cha miaka minane.
Habari za kufikiwa kwa makubaliano hayo zimesababisha kupanda kwa
bei ya mafuta ghafi kwa karibu asilimia 6.
Wanachama wa Opec wamekuwa wakilaumiana kusababisha mdororo wa bei
ya mafuta kutoka nana wao kushindwa kuchukua msimamo mmoja wa kudhibiti bei.
Wanachama wa Opec wamekuwa wakikutana Algeria.
"Opec imechukua uamuzi wa kipekee leo," waziri wa mafuta
wa Iran Bijan Zanganeh amesema.
Mafuta ghafi ya Brent, yanayotumiwa kama kigezo cha amfuta
kimataifa, yalipanda bei na kufikia karibu asilimia 6 hadi $49 kila pipa baada
ya tangazo hilo kutolewa.
Mawaziri wa mafuta wa nchi wanachama wamesema maelezo ya kina
kuhusu mwafaka wa sasa yatajadiliwa kwenye mkutano mwingine Novemba.
Uzalishaji wa mafuta utapunguzwa hadi mapipa 700,000 kwa siku,
ingawa upunguzaji wa uzalishaji hautakuwa sawa miongoni mwa wanachama.
Iran itaruhusiwa kuongeza uzalishaji wake.
Kulikuwa na suitafahamu awali baina ya Iran na mpinzani wake
Mashariki ya Kati Saudi Arabia, jambo ambalo lilikuwa limezuia kupatikana kwa
mwafaka.
Wazalishaji wadogo wa mafuta walipigania kupunguzwa kwa uzalishaji
baada ya mafuta kushuka bei kutoka $110 miaka miwili iliyopita.
Waziri wa mafuta wa Nigeria Ibe Kachikwu, taifa lililoathirika
sana, alisema huo ni "mkataba mzuri sana".
Waziri wa kawi wa Algeria Algerian Noureddine Bouarfaa amesema
uamuzi huo huo ulifikiwa kwa kauli moja.
Waziri wa kawi wa Qatar Mohammed Bin Saleh Al-Sada ambaye ndiye
rais wa sasa wa Opec amesema uzalishaji sasa utakuwa kati ya mapipa 33.2
milioni na 33 milioni kwa siku.
Uzalishaji wa sasa unakadiriwa kuwa mapipa 33.3 milioni kwa siku.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “BEI YA MAFUTA DUNIANI YAANZA KUPANDA BAADA YA MAAFIKIANO OPEC”
Post a Comment