Thursday, March 9, 2017
UN YAOMBA MATAIFA KUTOA MSAADA WA CHAKULA KWA WASOMALIA
Do you like this story?
Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) Antonio
Guterres ametoa wito kwa mataifa kutoa msaada wa chakula kwa raia wa
Somalia ili kupunguza baa la njaa linaloikabili nchi hiyo. Alitoa wito
huo Machi 7, 2017 katika zaiara yake ya dharula aliyoifanya nchini
Somalia.
Guterres alitoa wito huo baada ya
kushuhudia mateso makali wanayoyapata watu wenye utapiamlo na waathirika
wa ugonjwa wa kipindupindu alipotembelea wodi ya Baidoa iliyoko mji
mkuu wa nchi hiyo Mogadishu ikiwa ni mara ya kwanza kutembelea mji huo
tangu alipoteuliwa kuwa mkuu wa UN.
Amesema janga hilo linahitaji
kuchukuliwa hatua kubwa kutokana kwamba watu zaidi ya milioni sita ambao
ni sawa na nusu ya wakazi wa mji huo wanahitaji msaada hasa wa chakula.
“Kila mtu tuliyemuona alihadithia
mateso anayopata na hakuna namna ya kuelezea, watu wanakufa kwa njaa
dunia lazima ichukue hatua kukomesha janga hili,” alisema baada ya kuona waathirika wa kipindupindu katika wodi ya Baidoa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “UN YAOMBA MATAIFA KUTOA MSAADA WA CHAKULA KWA WASOMALIA”
Post a Comment